NHIF kuzipeleleza hospitali

Wednesday, May 22, 2013


Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa madai yanayotolewa kwao na wadau wao. Akizungumza katika mkutano na wadau wa Mbweni, Msimamizi wa NHIF wa Wilaya ya Kinondoni,Grace Mtemba alisema wameamua kufanya hivyo baada ya kupata malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wadau hao . “Tumepokea malalamiko mengi na hatua tunayoichukua sasa ni kutuma wapelelezi wetu katika hospitali zilizo lalamikiwa kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Mtemba.

Mkutano mkuu wa makandarasi kesho


Msajili wa Bodi hiyo, Mhandisi Boniface Muhegi aliyesimama
Bodi ya Usajili wa Makandarasi Nchini(CRB), itafanya Mkutano mkuu wake wa mwaka wa majadiliano kesho Dar es Salaam.
Msajili wa Bodi hiyo, Mhandisi Boniface Muhegi alitoa wito huo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano huo aliosema utaangalia kwa undani mafanikio na changamoto katika sekta ya ujenzi nchini kwa miaka 15 tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo. Alisema mkutano huo utakuwa na manufaa kwao ikiwamo kusaidia kuwapandisha madaraja na kupata alama katika maendeleo ya fani yao huku washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda na Rwanda wakialikwa kubadilishana uzoefu na washiriki wa ndani.

Mkutano wa JK, wabunge CCM waamsha makundi ya urais


Mkutano wa ndani baina ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete na wabunge wa chama hicho uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Dodoma, ni kama umeamsha upya makundi ya kuwania urais wa 2015, Mwananchi limebaini.
Kutokana na hali hiyo, jana chama hicho kililazimika kutumia nguvu kubwa kudhibiti taarifa zinazohusu kauli iliyodaiwa kuwa ilitolewa na Rais Kikwete, kwamba “Wanaoutaka urais kupitia CCM waanze kujipitisha ilimradi wasiwagawe wanachama kwa misingi ya makundi.”

CPwaa ateuliwa kuwa msimamizi

Thursday, May 16, 2013


Sharon Mariwa Meneja Muenezi Biashara Brainstormusic, Caroline Kakwezi, Meneja Masoko wa Heineken Tanzania na Uche Unigwe Mkurugenzi Mkuu na Cpwaa msanii maarufu wakishikana mikono na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania baada ya kusaini mkataba wa kuteuliwa kuwa msimamizi na MC wa michuano ya mpira wa mezani (Foosball) kulia ni Ronald Louis Meneja Opereshini wa Brainstormusic.

Huenda chelsea, Arsenal kucheza mechi kutafuta mshindi wa tatu




KLABU za Arsenal na Chelsea zinaweza zikamaliza Ligi Kuu ya England zikiwa zinalingana kwa kila kitu, pointi na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa hivyo kulazimika kucheza mechi maalum baina yao kutafuta timu ya kushika nafasi ya tatu.
Ushindi wa 4-1 wa Arsenal 4-1 dhidi ya Wigan unamaanisha The Gunners wamefikisha pointi 70 na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa 34, huku ikiwa imefunga mabao 71 msimu huu.

Kupanua Barabara Dar hadi Chalinze

Magufuli

Serikali imesema kwamba itapanua Barabara ya Morogoro kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze.
Akiwasilisha bungeni jana makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2013/14, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema lengo ni kupunguza msongamano wa magari na ajali.
Dk Magufuli alisema upanuzi wa barabara hiyo utaanzia Dar es Salaam na utakuwa wa umbali wa kilomita 200 na wizara imetenga kiasi cha Sh100 milioni kwa ajili ya maandalizi.

‘Mapepo’ yasababisha shule kufungwa


Wanafunzi wa Sekondari ya Kata ya Manzese, wamedai kutokewa na hali isiyoeleweka na kusababisha wenzao 32 kuanguka na kupoteza fahamu kwa nyakati tofauti.
Tukio hilo lilianza saa 2:35 asubuhi na kudumu hadi saa 6:00 mchana. Kutokana na hali hiyo, uongozi wa shule hiyo umesitisha masomo kutwa nzima ya jana ili kuwahudumia wanafunzi hao na kuwaruhusu wengine kurudi nyumbani hadi kesho.

Ripoti ya Elimu bungeni yaibua utata

Dk Shukuru Kawambwa

Kauli ya Serikali iliyotolewa bungeni juu ya kufutwa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na sababu za kufeli kwa wanafunzi wengi, imeibua utata baada ya taarifa kadhaa kuonyesha kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilibariki mabadiliko ya mfumo mpya wa kupanga madaraja.
Taarifa ya Serikali iliyosomwa bungeni Mei 3, mwaka huu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi ilisema Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), lilifanya mabadiliko ya mfumo bila kushirikisha wadau.