Mkutano mkuu wa makandarasi kesho

Wednesday, May 22, 2013


Msajili wa Bodi hiyo, Mhandisi Boniface Muhegi aliyesimama
Bodi ya Usajili wa Makandarasi Nchini(CRB), itafanya Mkutano mkuu wake wa mwaka wa majadiliano kesho Dar es Salaam.
Msajili wa Bodi hiyo, Mhandisi Boniface Muhegi alitoa wito huo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mkutano huo aliosema utaangalia kwa undani mafanikio na changamoto katika sekta ya ujenzi nchini kwa miaka 15 tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo. Alisema mkutano huo utakuwa na manufaa kwao ikiwamo kusaidia kuwapandisha madaraja na kupata alama katika maendeleo ya fani yao huku washiriki kutoka nchi za Kenya, Uganda na Rwanda wakialikwa kubadilishana uzoefu na washiriki wa ndani.
“Tunahamasisha ushiriki wa wakandarasi toka sekta binafsi na umma,” alisema Muhegi.
Alidokeza kuwa sekta ya ujenzi Tanzania imepiga hatua kubwa toka kuanzishwa kwa bodi hiyo ambapo sasa ina makandarasi 7000 ikilinganishwa na 1000 waliokuwapo miaka 15 iliyopita.Mengine ni kuongezeka kwa ubora na wingi wa kazi za ukandarasi wa ujenzi akitolea mfano ongezeko la minara ya mawasiliano ya simu za mkononi ambayo imetapakaa karibu nchi nzima, barabara na majengo ya k isasa.
Katika mkutano huo,mada nne zitawasilishwa kutoka kwa wadau mbalimbali zote zikilenga changamoto na mafanikio katika sekta ya ujenzi Tanzania ndani ya miaka15.

No comments:

Post a Comment

Tuachie Ujumbe wako hapa .