KLABU za Arsenal na Chelsea zinaweza zikamaliza Ligi Kuu ya England zikiwa zinalingana kwa kila kitu, pointi na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa hivyo kulazimika kucheza mechi maalum baina yao kutafuta timu ya kushika nafasi ya tatu.
Ushindi wa 4-1 wa Arsenal 4-1 dhidi ya Wigan unamaanisha The Gunners wamefikisha pointi 70 na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa 34, huku ikiwa imefunga mabao 71 msimu huu.
Hii inamaanisha ikiwa Chelsea itatoka sare ya bila mabao na Everton Uwanja wa Stamford Bridge katika mechi ya mwisho na kikosi cha Arsene Wenger kikaifunga Newcastle kwa wastani wa bao moja, iwe 2-1, 3-2, 4-3, timu hizo zitalingana kwa kitu.
Kwa kuwa nafasi ya tatu inaifanya timu ifuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa badala ya kuanzia kwenye kuwania kufuzu, inamaanisha kushika nafasi ya tatu ni hatua nzuri.

Uwezekano wa kumaliza msimu kwa mechi maalum ulipangwa zamani, rejea msimu wa 1995-96 wakati Manchester United na Newcastle United zilipokuwa zinagombea ubingwa. Licha ya mchuano mkali wa jino kwa jino, mwisho wa siku United ilishinda mbio za ubingwa bila mechi maalum. Chanzo: binzubeiry

I’m a Freelance Web Designer & Developer. I’m an enthusiastic, creative designer and geek with 3 years of strong commercial experience and a passion for creating beautiful, accessible websites using Web Standards
No comments:
Post a Comment
Tuachie Ujumbe wako hapa .