NHIF kuzipeleleza hospitali

Wednesday, May 22, 2013


Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) umeanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya uchunguzi wa madai yanayotolewa kwao na wadau wao. Akizungumza katika mkutano na wadau wa Mbweni, Msimamizi wa NHIF wa Wilaya ya Kinondoni,Grace Mtemba alisema wameamua kufanya hivyo baada ya kupata malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wadau hao . “Tumepokea malalamiko mengi na hatua tunayoichukua sasa ni kutuma wapelelezi wetu katika hospitali zilizo lalamikiwa kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Mtemba.
Naye Mfamasia Mshindo Busule,alisema wamekuwa wakipokea malalamiko mengi kutoka kwa wadau wao na kwa sasa wataifuta uanachama hospitali yoyote ambayo itakutwa na tuhuma hizo au kuwafikisha mahakamani itakapobidi.

No comments:

Post a Comment

Tuachie Ujumbe wako hapa .