"Muziki wa Tanzania unakufa", Duke

Thursday, March 14, 2013


Mtayarishaji wa muziki Duke kutoka studio za M Lab ambayo ndio iliwatoa wasanii kama Ben Pol, Grace Matata, Nikki Mbishi, One  Incredible na wengine wengi amesema kuwa muziki wa Tanzania umekufa.
Produza alisema hayo wakati akitoa maelezo ya yeye kuanzisha 'Kilinge' ambacho huwakutanisha wasanii wa wanaofanya muziki wa 'Hip Hop' na kuonyesha uwezo wao kila Jumamosi katika eneo la Msasani Club hapa jijini Dar es salaam.
Duke alisema kuwa dhumuni la kuanzisha 'Kilinge' ni kuhakikisha kuwa msanii anafanya kitu kwa ufasaha au kwa misingi inayotakiwa hii inaamisha kuwa si lazima mtu awe anafanya muziki wa 'Hip Hop' ndio afike hapo 'Kilingeni' au Cypher kwa lugha ya kiingereza kama watu wanavyodhani.
"Mtu yeyote yule ambaye anafanya muziki anaruhisiwa kufika ili tuwekane sawa na tujaribu kuufufua kwa kuelekezana". Mimi ni produza na pia kuna watu wengine wanajua kama ni muziki wa R&B unatakiwa uimbwe kwa njia zipi.
Hivi karibuni baba yake Dully Sykes alikuja nae hapa kushirikiana na sisi kwahiyo hii ni sehemu kwaajili ya kila mtu kuja kuonyesha uwezo wake na kuelekezana", Duke.
Alisema kuwa tangu waanzishe utaratibu huo wa kukutana kwenye Kilinge kila Jumamosi mpaka sasa ni miezi minne, baadhi ya wasanii wakongwe na wanaofanya vizuri waliofika ni Profesa Jay, Mapacha, Dan Msimamo, Izzo Biznes na wengine wengi.
Waanzilishi wa Kilinge ni Tamaduni Muziki ambao ni kama umoja unaoundwa na Produza Duke na wasanii kama Nikki Mbishi, Niite Songa, One Incredible na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment

Tuachie Ujumbe wako hapa .