Wema amnusuru Kajala jela

Tuesday, March 26, 2013


Wema Sepetu


MSANII mahiri wa filamu hapa nchini, Wema Sepetu, amemnusuru mwenzake Kajala Masanja, kwenda jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kifungo cha miaka minane au faini ya sh milioni 13.
Kajala alitiwa hatiani katika makosa ya kula njama kuhamisha umiliki wa nyumba iliyokuwa imezuiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali isiuzwe.

Chadema wasalimu amri kwa polisi, wasitisha maandamano

Monday, March 25, 2013




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekubali kusitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike leo kushinikiza kujiuzulu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012.
Makubaliano yalifikiwa baada ya kikao cha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Said Mwema na viongozi wa Chadema walioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kilichofanyika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

Mvua yasababisha kizaazaa Dar




Mvua kubwa iliyonyesha jana jijini Dar es Salaam, ilisababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo, hivyo nyumba kadhaa kujaa maji na baadhi ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.
Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua iliyoanza kunyesha muda wa asubuhi, pia yalisababisha hasara kubwa kutokana na vitu na mali mbalimbali kusombwa na maji.

A very funny pregnancy JOKE



Four men are in the hospital waiting room because their wives are having babies. A nurse goes up to the first guy and says, 

“Congratulations! You’re the father of twins.”

“That’s odd,” answers the man. “I work for the Minnesota Twins!”

Waziri Sitta awaanika wabunge wa Afrika Mashariki kuhusu posho

Saturday, March 23, 2013



Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewajibu wabunge wa Afrika Mashariki akisema wengi hawahudhurii vikao vya kupewa mwongozo kuhusu bunge hilo kwa kuwa “wanataka kulipwa posho”.

Kauli hiyo ya Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, imekuja siku moja tangu wabunge hao waichongee wizara hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, kwamba imeshindwa kuwapa mwongozo pale wanapokwenda kwenye vikao vya Bunge la Afrika Mashariki.

Watuhumiwa 17 Tazara wasimamishwa kwa uchunguzi

Thursday, March 21, 2013




Wafanyakazi 17 wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya kuhusishwa na tuhuma za kusafirisha mizigo kwa njia ya magendo kupitia treni ya uokoaji.
Mizigo hiyo ni mbao na mkaa iliyokuwa imehifadhiwa kwenye mabehewa sita ya treni hiyo, ikitokea eneo la Mzenga, wilayani Kisarawe, Pwani usiku wa kuamkia Jumapili.
Gharama za kusafirishia mizigo hiyo ilikuwa ni Sh12 milioni. Kaimu Mkurugenzi wa Tazara, Dk Damas Ndumbaro alisema hatua hiyo ni kupisha uchunguzi.

CCM, Chadema Dar wamgeuzia kibao JK

Mh. JK Kikwete


Dar es Salaam. Ni nadra kutokea lakini wafuasi wa vyama vya siasa vya CCM na Chadema, wameungana kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu kero ya maji eneo la Kimara-Golani, Dar es Salaam.
Rais Kikwete alikutana na hali hiyo wakati akifungua Daraja la Kimara jana, tukio hilo liliwakusanya watu wengi hasa wanachama wa CCM na Chadema waliokuwa wamevalia sare za vyama vyao.

Wanafunzi washinda danguroni Dar




Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Majani ya Chai iliyopo Kipawa jijini Dar es Salaam, wametajwa kujiingiza katika kashfa ya ngono, kuvuta na kuuza bangi katika moja ya nyumba zinazozunguka shule hiyo.
Hilo ni tukio lingine jipya, kwani mwishoni mwa mwaka jana, kuliibuka matukio ya ajabu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi, Ruaruke, Rufiji mkoani Pwani ambao walielezwa kujihusisha na uvutaji bangi hata kukonyeza na kubaka walimu wao.
Mkuu wa Sekondari hiyo, Jasinta Assey alikiri na kusema kwamba vitendo vya uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake, vinachangiwa na askari wa Kituo kidogo cha Stakishari ambao alidai wanachukua rushwa kwa wauzaji wa bangi na nyumba bubu za wageni. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Shule hiyo, Jasinta Assey alisema ni kawaida ya polisi hao kwenda kwenye nyumba hizo kunakofanyika biashara hizo na kuchukua rushwa badala ya kutatua tatizo.
Alisema ongezeko la utoro katika shule hiyo ni tatizo kubwa na wanafunzi wa kidato cha nne wanaosoma masomo ya sanaa ndiyo wanaoongoza kwa kuvuta bangi na kwenda kufanya ngono katika nyumba zilizo jirani na eneo la shule hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema hajapata taarifa za hali hiyo.
“Ngoja nimtume Mkuu wa Kituo cha Polisi Stakishari afuatilie kwa karibu,” alisema Minangi na kuongeza: “Lakini ngoja nikwambie, hili suala nakumbuka liliwahi kuripotiwa 2011 wakati nikiwa mkuu wa kituo hicho; nililishughulikia na tulibaini kuwa hakuna mwanafunzi ambaye alikuwa anaenda kwenye nyumba hizo kuvuta bangi wala kufanya ngono.
“Kilichotokea kwa wakati huo ni kwamba, tuliwachukua baadhi ya wanafunzi ili watupeleke mahali walipokuwa wakifanyia vitendo hivyo kutokana na maelezo na vielelezo vyao, lakini hatukubaini hizo sehemu.

“Inawezekana basi haya mambo yameibuka upya baada ya kuona kuna mkuu wa kituo mwingine mpya,” alisema Kamanda Minangi.
Kutokana na matendo hayo, wanafunzi wengi walifanya vibaya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka jana.

“Walifeli sana mwaka jana hawa, walimu wapo, tunawapa nyenzo lakini hawataki, ninaiomba Serikali kuingilia kati suala hili kwani ni la muda mrefu na ni faida ya vijana hawa,” alisema.

Shule ya Majani ya Chai ilishika nafasi ya 61 kimkoa kati ya shule 226 wakati ngazi ya taifa, ilishika nafasi ya 543 kati ya shule 3,392.

Wanafunzi 274 walijisajili kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana na kati yao 130 walipata sifuri, wakati waliopata daraja la nne ni 85, waliopata Daraja la Tatu ni 18 wakati waliopata daraja la pili ni watano. Hakukuwa na daraja la kwanza na wanafunzi 36 hawakufanya mtihani.

“Baada ya kuona utoro umekithiri shuleni hapo, nilikwenda kutoa taarifa kituo kidogo cha Polisi Stakishari, lakini hawakuonyesha ushirikiano matokeo yake wanakwenda kwa wenyeji hao na kuchukua rushwa.

“Hili inaonekana kama ni dili la hawa askari, kwani wapo walionifuata na kunieleza niache kufuatilia, lakini mimi niliwaambia nitafuatilia tu na ilifikia hatua nikatishiwa maisha.
“Baada ya kuona nazidi kutishiwa maisha, niliogopa, nikaacha...na hivi ninavyoongea na wewe, najua tu watanifuata kwani nimeshaambiwa nikipita peke yangu eneo wanakofanyia biashara zao watanifanyia kitu kibaya,” alisema Assey.

Taasisi ya Mkapa kujenga nyumba 700 vijijini




Taasisi ya Mkapa Foundation, inatarajia kujenga  nyumba  700 za watumishi wa afya wanaotoa huduma  katika maeneo ya vijijini.
Hatua hiyo inalenga katika, kuwaboreshea mazingira mazuri watumishi hao ili waweze kutoa huduma kwa ufanisi.
Hayo yalibainishwa juzi na Ofisa Mipango wa Kitengo cha Uwezeshaji  katika taasisi hiyo, Pamela Maro, alipokuwa akizungumzia shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo katika kuboresha huduma za afya vijijini.
Alisema lengo la ujenzi wa nyumba hizo ni kuboresha huduma kwa wananchi wa  vijijini wanaokabiliwa na changamoto nyingi.
Maro alisema  taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii  kuhakikisha kuwa changamoto zinazowakabili wananchi wao vijijini zinatatuliwa.
Alisema mbali na  kujenga nyumba hizo  taasisi hiyo pia imekuwa ikiisaidia Serikali kwa kuipatia watumishi wa afya na kuwapeleka katika maeneo ya vijijini.
Alisema tayari taasisi imeshaisaidia Serikali watumishi 230 wa sekta hiyo ambao wamepelekwa katika vituo  mbalimbali vya afya na  hospitali za wilaya.
Ofisa huyo alisema katika kuhakikisha kuwa huduma zinaboreka zaidi, taasisi imekuwa ikitoa  mafunzo mbalimbali kwa timu za wasimamizi wa afya walioko wilayani.
Maro alisema mafunzo hayo pia yametolewa kwa wasimamizi wa vituo vya afya katika mikoa mbalimbali.
Alisema pamoja na jitihada hizo, lakini tatizo la uhaba wa watumishi katika vituo na hospitali mbalimbali ni kubwa sana.

Sababu za Ntaganda kujisalimisha Marekani

Kiongozi wa wapiganaji wa M23 Jenerali Bosco Ntaganda  aliyejisalimisha katika ubalozi wa Marekani mjini  Kigali.



Kutoka Kongo.
Kiongozi wa wapiganaji wa M23 ambao wamekuwa wakipambana dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC), Jenerali Bosco Ntaganda amejisalimisha katika Ubalozi wa Marekani mjini Kigali, ikielezwa kwamba uamuzi huo unatokana na kuhofia usalama wake.
Hatua hiyo ilitokana na kushindwa kwa Ntaganda na kamanda mwingine wa waasi, Sultan Makenga siku ya Jumamosi baada ya wiki kadhaa za msuguano ndani ya M23, kundi la waasi la hivi karibuni kuongozwa na Watutsi dhidi ya Serikali ya mbali.
Uasi wa M23 katika Mkoa wa Kivu Kaskazini wenye utajiri mkubwa wa madini, ulisababishwa na mipango ya Rais Joseph Kabila kumkamata Ntaganda na kumkabidhi kwa ICC. Taarifa zinaeleza kwamba kiongozi huyo aliamua kujisalimisha kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Rwanda, baada ya kuripotiwa kuvuka mpaka Jumamosi iliyopita, ambapo Serikali ya Rwanda ilikana kumkamata.
Shirika la habari la AFP lilieleza kwamba Ntaganda aliamua kujisalimisha baada ya kundi la wapiganaji alilokuwa akiliongoza kuzidiwa nguvu kutokana na vita ya ndani iliyoligawanya Kundi la M23.
Ntaganda alikuwa kiongozi wa kijeshi aliyemuunga mkono aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa kundi la M23 Jean Marie Runiga ambaye aliripotiwa kukamatwa Jumamosi na kuhifadhiwa sehemu maalumu baada ya kukamatwa na wanausalama wa Rwanda alipovuka mpaka kuingia nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Rwanda, Ntaganda aliamua kujisalimisha kwa Ubalozi wa Marekani mjini Kigali kwa kuhofia usalama wake iwapo angeingia mikononi mwa Serikali ya Rwanda.
Mmoja wa maofisa wa Jeshi la Rwanda ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kwamba, “Nina uhakika kwamba anatuogopa sisi kuliko anavyoiogopa Marekani kwa sababu amekuwa akitusababishia migogoro mingi na jirani zetu.”
Ofisa huyo alisema kwamba maelezo ya awali yaliyokuwa yakitoka kwa watu wake wa karibu yalikuwa yakieleza kwamba alikuwa amepotolea misituni lakini yalikuwa yakitiliwa shaka na wanausalama wa Serikali ya Rwanda.
Kwa kujisalimisha mjini Kigali, ambako ofisa mmoja wa ubalozi alisema wafanyakazi walishtushwa na kuwasili kwake kwa ghafla, Ntaganda amehitimisha safari ndefu iliyomshuhudia akipigana kama muasi na mwanajeshi wa Serikali kwa pande mbili za mpaka wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, wakati wa mgogoro wa karibu miaka 20 katika Kanda ya Maziwa Makuu.Uwepo wa Ntaganda ulikuwa haujulikani baada ya mamia ya wapiganaji wake kukimbilia nchini Rwanda na wengine kujisalimisha kwa Umoja wa Mataifa mwishoni mwa wiki, baada ya kushindwa kwake na kundi hasimu la M23 walilojitenga nalo.
Msemaji wa ICC, Fadi El-Abdullah alisema mahakama hiyo itachukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha kuwa mtuhumiwa huyo anafikishwa haraka mjini The Hague na kuongeza kuwa hakuna kizuizi kwa taifa lisilo mwanachama wa mahakama hiyo kushirikiana nayo kwa msingi wa kujitolea.
Rwanda na Marekani zote siyo wanachama wa ICC na kwa hivyo haziwajibiki kumkabidhi Ntaganda, lakini Nuland alisema nchi yake inaunga mkono.

Prezzo afunguka kuhusu Goldie

Wednesday, March 20, 2013

Prezoo


Tangu kurudi kwake Nigeria, na kutengwa kuhudhuria mazishi ya anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Goldoe Harvey nyota wa Big Brother toka nchini Kenya, John Makini anayejulikana zaidi kwa jina la Prezzo hajasema lolote kwa vyombo vya habari kuhusiana na majanga yaliyompata huko.
Prezzo, alikuwa Nigeria ambako alikwenda kwa ajili ya Sikukuu ya Wapendanao na kukutana na kifo cha mshiriki mwenzake wa Big Brother na mwanamuziki Mnaijeria, Goldie Harvey ambaye inaaminika walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Kilichokuja kuibuka na kumchanganya zaidi Prezzo ni mtu anayejulikana kwa jina la Andrew Harvey ambaye aliachia mtandaoni picha za harusi yake na mwanadada Goldie Harvey, ambaye pia siku chache zilizopita alionekana Nigeria akihudhuria mazishi ya mwanadada huyo.
Prezzo kwa upande wake, aliwaambia wanahabari kwamba anahitaji muda wa kupumzika kabla ya kusema lolote.

Mwamvita Makamba Amjulia hali Absalom Kibanda

 
 
Mwamvita Makamba, akiwa katika chumba alicholazwa Mhariri Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri wakati alipomtembelea kumjulia hali katika Hospitali ya Milpark baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo jana usiku nchini Afrika ya Kusini

Watanzania watakiwa kujenga hoteli za kitalii

Mh Nyalandu


WAJASIRIAMALI nchini, wametakiwa kujenga hoteli za kitalii kwa lengo la kukabiliana na tatizo kubwa la uhaba wa vitanda katika hoteli hizo.
Naibu Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu alitoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati akizundua hoteli ya kitalii ya Palace ambayo imejengwa kwa ubia na Shirika la Nyumba Nchini(NHC).
Lazaro alisema uwekezaji huo utasadia kuongeza idadi kubwa ya watalii na  mapato nchini.
“Mwaka jana tulipata watalii 800,000 ukilinganisha na Rwanda ambayo ilipata 600,000 licha kuwa nchi ndogo,  tatizo kubwa la nchi yetu ni upungufu wa vyumba vya kulala wageni,”alisema Nyarandu.
Alisema ujenzi huo utasaidia Mkoa wa Arusha kuongeza idadi ya vitanda vya kisasa vya kulala wageni. Mkoa wa Arusha sasa una  jumla ya vitanda 2,800  tu, nyuma ya Mkoa wa Dar es salaam wenye vitanda 3,800 wakati Mkoa wa Mwanza una vitanda 900 licha ya ukubwa wake.
“Tunaomba shirika la nyumba lijitanue kwa kujenga hoteli za kisasa za kitalii, sisi wizara tunahitaji wawekezaji wa ndani na nje wajitokeze kujenga katika maeneo ya wazi na ndani ya hifadhi zetu, tumejipanga kukabiliana na watumishi wanaokwamisha watu wenye nia njema,”alisisitiza.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu  alisema ujenzi wa hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota nne, umegharimu Sh16 bilioni na NHC imetoa ardhi na Sh9 bilioni huku kiasi kingine kikitolewa na Palace Hoteli.
Alisema mradi wa hoteli hiyo ni moja ya miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa, kutokana na uwazi wa kuendesha hoteli hiyo na hivyo kuingiza mapato kwa pande zote NHC na mbia.
Naye Dk Macha alisema mradi huo hadi sasa umetoa ajira kwa wafanyakazi 120 na unatoa huduma nyingine kadhaa, ikiwamo huduma za kibenki na utachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa Mkoa wa Arusha na Taifa.
Akifungua mradi huo rasmi, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka alipongeza mradi huo na kutoa wito kwa wajasiriamali kujitokeza na kuingia ubia na NHC katika kutekeleza miradi mbali mbali.
Alisema mradi huo unakwenda vizuri na umeongeza mapato ya NHC kwani katika eneo hilo, kabla ya ujenzi wa hoteli walikuwa wakipata kwa mwaka Sh31 milioni pekee, lakini sasa wanapata Sh151 milioni.

Ofisa usalama mbaroni wizi kontena

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.



VIGOGO watano akiwamo Ofisa wa Usalama wa Taifa wanashikiliwa polisi, kwa tuhuma za kutaka kusafirisha kontena la madini aina ya Tantalite yenye thamani ya Dola 22,000 za Marekani yaliyokuwa  yakisafirishwa nje ya nchi.
Akizungumza na Dar es Salaam jana, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliapa kuilinda Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa udi na uvumba.
Kiapo hicho alikitoa jana wakati akiwataja watu  wanaoshikiliwa na polisi kwa kuichafua TPA,  wakati yeye akifanya jitihada za kuisafisha.
Aliwataja watu hao  kuwa ni Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mmiliki wa Kampuni ya Uwakala wa Kusafirisha Mizigo ya GFC na msaidizi wake.
Wengine ni  Ofisa wa Mamlaka ya Ukaguzi Madini (TMAA),  Mmiliki wa Bandari Kavu na Ofisa wa Usalama  wa Taifa.
Dk Mwakyembe alisema mzigo huo uliokamatwa ukitaka kusafirishwa kwenda nje ya nchi,  madini yake aina ya Tantalite hayapatikani nchini, bali nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Alisema walibaini katika nyaraka  zinazohusiana na kusafirishwa kwa madini hayo kuwa, zinaonyesha madini hayo yanatoka nchini wakati siyo kweli.
Kuhusu Ofisa wa Usalama wa Taifa, Mwakyembe alisema ni mtu muhimu ambaye taifa linamwamini kuficha siri za nchi, lakini akashangaa kuwamo kwenye mlolongo huo.
“Yaani sisi tunafanya kazi ya kuisafisha bandari, watu hawa wanaichafua kuifanya kuonekana ni uchochoro wa kusafirisha magendo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Kutokana na hili, kampuni mbili za meli za Safmaline na Maikesi zimesitisha kusafirisha mizigo yao, kutokana na michezo michafu kama hii, watu siyo waaminifu wanabadilisha mizigo halisi  kama madini wao wanaweka simenti au magadi ambayo yana uzito sawa na mzigo halisi.”
Aliongeza kuwa mmiliki wa Bandari Kavu ya PMM na mtendaji wake mkuu nao pia wanahojiwa  polisi kutokana na tuhuma hizo.
Kuhusu mfanyakazi wa TRA, Dk Mwakyembe alisema ndiye aliyetoa ridhaa ya mzigo huo kusafirishwa  kwa magendo.
Pia, Dk Mwakyembe alisema amewaagiza maofisa wa polisi kumtafuta raia wa Congo aliyepeleka mzigo huo bandarini, kwa lengo la kuusafirisha  kwenda  nchini Romania.

Wakaguzi hesabu 75 wapata kazi UN

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Tanzania,Ludovick Utoh

Wakaguzi 75 wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (Naot), wataondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu kwenda nchi mbalimbali kufanya ukaguzi wa hesabu za mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN). Mwaka 2011, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh aliteuliwa kuwakilisha Afrika kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakaguzi wa Hesabu za UN na kwamba, moja ya majukumu ya Naot ni kufanya ukaguzi katika mashirika ya umoja huo. Akizungumza mjini Bagamoyo jana, Utouh aliwataka kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi yao.

12 wafa ajalini Mwanza, Mbeya



Mwanza na Mbeya. Watu 12 wamefariki katika ajali mbili tofauti zilizotokea katika Mikoa ya Mbeya na Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alisema kati ya hao sita waliofariki, wamo raia watano wa Malawi huku wengine 25 wakijeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la ‘Easy Bus’ aina ya Scania kupinduka katika Kijiji cha Igawa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Waliofariki na kutambuliwa katika ajali hiyo ni pamoja na Atham Bonzo, Maria, Adam, Sakwati na mtoto mdogo anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja ambao wote ni wakazi wa Malawi. Pia Rajabu Hassan (35), mkazi wa Tanga aliyekuwa kondakta wa basi hilo.

Kamanda Diwani alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika Barabara ya Mbeya-Iringa saa 3:30 asubuhi. Awali ilielezwa kwamba Chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na basi la Taqwa lililokuwa likiendeshwa na Kenneth Thomas (48) mkazi wa Kabwe jijini Mbeya.

Alisema kuwa dereva wa basi hilo la Taqwa lililokuwa likitokea Malawi kwenda Dar es Salaam alikuwa akijaribu kulipita basi la Easy na baada ya kulipita alikutana na gari lingine kwa mbele na ndipo dereva wa basi hilo alipochukua uamuzi wa kurudi nyuma.

“Dereva wa Taqwa aliporudi nyuma ndipo dereva wa basi la Easy, Ajali Mohamed (32) mkazi wa Iringa alipopoteza mwelekeo na kuacha njia na kupinduka na kusabaisha vifo vya watu hao,” alisema.

Kamanda Athumani alisema kuwa dereva wa basi la Taqwa anashikiliwa na polisi wakati taratibu za kumfikisha mahakamani zikifanyika wakati mwenzake wa Easy alikimbia baada ya tukio hilo.

Alisema kuwa miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kwamba majeruhi 25 wakiwamo wanaume 14 na wanawake 11 wamelazwa katika Hospitali ya Mission ya Ilembula na wanaendelea na matibabu.

Katika ajali nyingine, basi la Mkwizi linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Musoma, liligongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa na mchanga katika eneo la Igoma wilayani Nyamagana mkoani Mwanza na kusababisha watu sita kufariki dunia papo hapo.
Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa dereva wa basi pamoja abiria wawili waliokuwa wamekaa viti vya mbele walifariki huku ikielezwa kuwa dereva wa Fuso pamoja na watu wengine wawili waliokuwamo ndani yake nao walikufa papo hapo.

Chanzo cha ajali hiyo imeelezwa kuwa ni askari wa usalama barabarani, aliyekuwa amesimamisha magari zaidi ya matatu.

“Alisimamisha lori la kwanza la Fuso wakati lori jingine la aina hiyo likiwa nyuma na ndiyo lilikutana uso kwa uso na basi na kufanya askari hao kutoweka,” alieleza Salum Bakari, ambaye alishuhudia ajali hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Elias Mangu alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema bado anasubiri taarifa rasmi kutoka kwa maofisa wake waliokwenda eneo la tukio.

Audio Track: Diamond Platinumz - Kesho



Song: Kesho
Studio: Mj-Recordz

{Chorous}
=i> Mi nataka kesho twende nikupeleke nyumbani
nataka kesho twende ukamuone mama x2

{Verse 1}
=I> Kwanza kabisa ntanyonga Tai
T"shirt na Jeans ntatupa kidogo..
Unite Nasibu usiniite Dai
Asije kukuona muhuni akapandisha Mbogo...
Naukifika uagize Chai
Savanna Takila uzipe kisogo...
Kuhusu mavazi kimini haifai
Tupia pendeza ila za Hekima Logo...
=I> Even though wanaponda eti we ni kicheche
Waambie ndoo chaguo langu sasa wanicheke x2

Chorous}
=I> Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2

{Verse 2}
Usilete swaga za Nainai
Ukanyoa kiduku kama Moze Iyobo..
Eti shoping twende Tai
wakati Dadaangu anaduka kigogo..
Ukikuta Nguna usikatae
we zuga unapenda hata kama wa Muhogo..
Kuhusu kabila mbona Sadai
Mama angu hana noma hata kama Mgogo
=I> Even though wanaponda eti we ni kicheche
Waambie ndoo chaguo langu sasa wanicheke x2

{Chorous}
=I> Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2

Bridge
Mama yangu mama...
Mama Naseeb mama...
Mama Diamond mama...
Mama yangu nyumbani...
Mama Chali mama...
Mama Sepetu mama...
Mama Kidoti mama...
Kwa mama Diamond nyumbani...

{Chorous}
=I> Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2

Audio Track: Diamond Platinumz - Nataka Kulewa






Song: Kulewa

Studio: Am Records

We niache niende niende niende ni ende x2

{Verse 1}

Usiniulize kwanini sababu utanizingua

ukitakajiunge na mimi kama ni pesa we kunywa ntanunua...

Mi mwanzo sikuamini nikajuaga vyakuzua

Kumbe mjinga ni mimi ninayetunza wenzangu wanachukuwa..

(Oooh! Mapenzi) Mapenzi yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya,

mie siwezi kwa yalonikuta we niache niseme jina

(Ooooh! Mapenzi) yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya

na nnamengi yamenikaa moyoni

{Chorous}

Leo nataka kulewa {Lewaaaaa}

Mi nataka kulewa {Lewaaaaa}

Nataka kulewa {Lewaaaaa}

Zikipanda nimwage radhi....x2

We niache niende niende niende ni ende...x2

(Vearse II)

Mi kwa mapenzi maskini Nikamvisha na pete nikamuoa

kukata vilimilimi vya wazushi wanafki wanaomponda...

kumbe mwenzangu na mimi ni bure tu najisumbua

si tuko kama ishirini mabuzi ving`asti wengine anawaonga..

(Oooh! Mapenzi) yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya,

mie siwezi, kwa yalonikuta we niache niseme jina

(Ooooh!) Mapenzi yalinifanya ka_mtoto nilie vibaya

na nnamengi yamenikaa moyoni

{Chorous}

Leo nataka kulewa {Lewaaaaa}

Mi nataka kulewa {Lewaaaaa}

Nataka kulewa {Lewaaaaa}

Zikipanda nimwage radhi....x2

We niache niende niende niende niende..x2

Audio Track: Dully Sykes, Diamond & Ommy Dimpoz - Utamu












Audio Track: Nay wa Mitego ft Diamond : Muziki Gani




Audio Track: Juma Nature ft Tundaman - Haipotei




Lwakatare kizimbani kwa ugaidi, kula njama kumdhuru mwanahabari

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Willfred Lwakatare (wapili kulia) na Ludovick Rwezahura (kulia) wakiondolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na askari kuelekea kupanda gari kwa ajili ya kurudishwa rumande, Dar es Salaam, jana.


Dar es Salaam. Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Rwezaura wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu waki kabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kula njama ya kutenda kosa la jinai la kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, Wakili wa Serikali Mkuu, Prudence Rweyongeza kuwa washtakiwa hao walifanya kosa la kula njama na kutenda makosa ya jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28, mwaka jana katika eneo la King’ong’o katika wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama kwa kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Msacky, kinyume na kifungu cha 227 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Wakili huyo wa Serikali katika shtaka la pili alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kufanya kosa la jinai kinyume na kifungu cha sheria cha 24 (2) cha Sheria dhidi ya Ugaidi, sura ya 21 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai kuwa washtakiwa hao, Desemba 28, 2012 walishirikiana kupanga njama za utekaji nyara dhidi ya Msacky kinyume na kifungu cha 21 cha sheria inayopinga ugaidi.
Katika shtaka la tatu, washtakiwa hao wanadaiwa kufanya mkutano wa vitendo vya kigaidi, kinyume na kifungu cha 5 (a) cha sheria namba 21 inayopinga ugaidi iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Aliendelea kudai kuwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa hao walipanga na kushiriki katika mkutano wa kupanga kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara dhidi ya Msacky.
Kwa mujibu wa shtaka la nne, Lwakatare anadaiwa kuhamasisha vitendo vya ugaidi.

Aliongeza kudai kuwa siku hiyo ya tukio, Lwakatare akiwa mwenye nyumba, akijua, aliruhusu mkutano kati yake na Ludovick ufanyike katika nyumba yake kwa lengo la kuhamasisha vitendo vya kigaidi dhidi ya Msacky.

Baada ya kumaliza kusoma mashtaka hayo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

“Mheshimiwa Hakimu kesi yoyote inayohusiana na vitendo vya kigaidi haina dhamana,” alisema Rweyongeza.Rweyongeza pia aliiomba Mahakama kuruhusu mshtakiwa Ludovick kurudishwa polisi kuendelea na shughuli za upelelezi.

Lwakatare anatetewa na mawakili, Peter Kibatala, Mabere Marando, Abdallah Safari, Nyaronyo Kichere na Tundu Lisu.

Wakili wa utetezi, Kibatala aliiomba Mahakama kutoa dhamana kwa mteja wao kulingana na mazingira husika na kwamba izingatie kuwa dhamana ni haki ya msingi ya mshtakiwa.
“Ugaidi siyo kosa dogo ni kitu kikubwa iwapo chombo cha kisheria kinachukua haki ya mtu ya dhamana ni lazima kuwapo na sababu zinazojitosheleza kuwa mtu huyu kweli ni hatari na Mahakama iridhie kweli ni hatari na anyimwe dhamana,” aliongeza Kibatala.

Wakili Lissu aliunga mkono hoja za wakili Kibatala.
Kwa upande wa wakili Safari aliitaka Mahakama ichukue kumbukumbu kuwa vitendo vya kubambikia kesi watu vimekithiri katika nchi hii.
Hakimu Mchauro atatoa uamuzi kesho Jumatano kama washtakiwa hao watapata dhamana ama la.

Sitta alaumu mawaziri kwa kugeuzwa chambo

Mh Samwel Sitta

 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema idadi ndogo ya walipa kodi nchini inachangiwa na  baadhi ya mawaziri kutumika kama chambo cha ukwepaji walipa kodi.         
Akizungumza kwenye Siku ya Ustawi wa Jamii jana, Sitta alisema  Tanzania ina watu milioni 45, lakini walipa kodi ni milioni moja.
Alisema wengi hukwepa kwa kutumia mianya ya viongozi waliopo madarakani, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya nchi.
Pia, Sitta alisema suala la kujuana na uongozi wenye ulafi na ubinafsi, unaonekana kuchangia kwa  kiasi kikubwa suala la umaskini kuendelea kuitesa nchi.
Alisema hali hiyo inasababisha tabaka moja la viongozi kufaidi keki ya Watanzania, huku idadi kubwa ya wananchi wakisalia kuogelea kwenye dimbwi la umaskini. Waziri Sitta alisema viongozi walafi na waotumia vyeo vibaya kufuja mali za umma, hutoa mfano mbaya  kwa watendaji wengine wanaohudumia watu wenye mahitaji.
Alisema chanzo cha matatizo mengi ya watoto, umaskini, ukosefu wa usawa na mengine ni matokeo ya uchumi mdogo.

Lowassa afufua kashfa ya kigogo Ikulu

IKULU

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.

Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.

Mpango huo unadaiwa kusukwa Juni mwaka jana kwa maofisa haokuitaka Wizara ya Fedha kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya safari hewa ya Rais.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.

Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.

Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.

Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.

“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.

Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.

Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

Diamond tena! ..apangua tuhuma moja baada ya nyingine

Thursday, March 14, 2013


MSANII anayeaminika kuwa na nyota ya kupendwa na mashabiki na wadau wengi wa muziki wa kizazi kipya hasa wanawake, Naseeb Abdul au Diamond Platinumz kama anavyojiita,  amejitokeza kujibu tuhuma kadhaa zinazomkabili.
Hatua hiyo imekuja baada ya maswali mengi kuibuka na shutuma nyingi kumwangukia kupitia vyombo mbalimbali vya habari, huku akiwa amekaa kimya, kiasi cha kufanya baadhi ya watu kutoelewa ni kwa nini ameamua kutozungumza chochote.
Moja ya tuhuma kubwa inayomkabili ni kuhusiana na mganga wa kienyeji anayehangaika kwenye vyombo vya habari na kudai kwamba amemfikisha Diamond hapo alipo lakini kwa sasa amekimbiwa na msanii huyo.
Akijibu tuhuma hiyo akasema kwamba kwanza hamjui huyo mganga, ila kiukweli ni kwamba  kuna watu wanataka kumchafua, na kama ni mganga kweli na kakimbiwa na mteja aliyempandisha kwa nini asitumie uganga kumshusha?
"Mganga wa kweli jamani hawezi kukimbilia kwenye vyombo vya habari, mganga wa kweli anamalizana na mteja kimya kimya na mteja mwenyewe anajikuta anarudi kwa mganga kuomba radhi, huyu sio mganga, ingawa simjui!”
Tuhuma ya pili ni kuhusiana na maonyesho yake kudorora ambapo pia mganga huyo amehusishwa, kwamba yeye ndiye aliyemlaani na kusababisha mambo ya mwanamuziki huyo anayefikiriwa kuwa ni tajiri kuliko wenzake, kuanza kwenda mrama.
Jibu alilolitoa ni kwamba hakuna jambo lake hata moja linalokwenda vibaya. Picha zilizochapishwa na gazeti moja la kila wiki, likionyesha ukumbi ukiwa mtupu katika onyesho ambalo alilifanya Arusha, zilipigwa mwanzoni, wakati hapakuwa na mashabiki wengi waliokuwa wameingia, ukumbi baadaye ulijaa.
"Na kama ni maonyesho, nina ratiba ya show mpaka mwezi wa saba, sasa nimeshuka vipi jamani?", alisema huku akionekana mwenye masikitiko makubwa kwa kile anachosema anaonewa tu na maneno hayo ya uzushi.
Habari nyingine kubwa iliyoenea mjini ni ile inayohusiana na uhusiano wake na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Entertainment Masters, Peniel Mungilwa ambapo katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakionekana mara kwa mara wakiweka picha zao zinazoonyesha dhahiri wapo katika mapenzi.
Hili alionekana kama kushtushwa nalo ingawa baadaye alijiweka sawa na kusema ni sinema tu za hapa na pale lakini si ukweli kwamba wana uhusiano.


"Muziki wa Tanzania unakufa", Duke


Mtayarishaji wa muziki Duke kutoka studio za M Lab ambayo ndio iliwatoa wasanii kama Ben Pol, Grace Matata, Nikki Mbishi, One  Incredible na wengine wengi amesema kuwa muziki wa Tanzania umekufa.
Produza alisema hayo wakati akitoa maelezo ya yeye kuanzisha 'Kilinge' ambacho huwakutanisha wasanii wa wanaofanya muziki wa 'Hip Hop' na kuonyesha uwezo wao kila Jumamosi katika eneo la Msasani Club hapa jijini Dar es salaam.
Duke alisema kuwa dhumuni la kuanzisha 'Kilinge' ni kuhakikisha kuwa msanii anafanya kitu kwa ufasaha au kwa misingi inayotakiwa hii inaamisha kuwa si lazima mtu awe anafanya muziki wa 'Hip Hop' ndio afike hapo 'Kilingeni' au Cypher kwa lugha ya kiingereza kama watu wanavyodhani.
"Mtu yeyote yule ambaye anafanya muziki anaruhisiwa kufika ili tuwekane sawa na tujaribu kuufufua kwa kuelekezana". Mimi ni produza na pia kuna watu wengine wanajua kama ni muziki wa R&B unatakiwa uimbwe kwa njia zipi.
Hivi karibuni baba yake Dully Sykes alikuja nae hapa kushirikiana na sisi kwahiyo hii ni sehemu kwaajili ya kila mtu kuja kuonyesha uwezo wake na kuelekezana", Duke.
Alisema kuwa tangu waanzishe utaratibu huo wa kukutana kwenye Kilinge kila Jumamosi mpaka sasa ni miezi minne, baadhi ya wasanii wakongwe na wanaofanya vizuri waliofika ni Profesa Jay, Mapacha, Dan Msimamo, Izzo Biznes na wengine wengi.
Waanzilishi wa Kilinge ni Tamaduni Muziki ambao ni kama umoja unaoundwa na Produza Duke na wasanii kama Nikki Mbishi, Niite Songa, One Incredible na wengine wengi.

Hemed 'PHD' kutoka na filamu saba peke yake


Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki na filamu pia Hemed Seif Suleiman aka PHD, amesema kuwa mwaka huu hatoigiza sana kwenye filamu za watu kwasababu ameingia mkataba na kampuni moja ya usambazaji ambayo inamtaka kutengeneza filamu zake mwenyewe 7 kwa mwaka.
Hemed alisema kuwa mkataba huo utamfanya yeye kufikiria zaidi filamu zake kuliko kucheza kwenye filamu za watu wengine.
Hemed alieleza kuwa ubize huo wa mwaka pia ndo unamfanya kushindwa kuanza kutengeneza nguo za ndani za wanawake kama alivyosema mwaka huu kuwa anatarajia kuanza kubuni nguo zake za kike za ndani za wanawake.
Alisema kuwa bado mipango ya nguo hizo iko palepale kama ilivyokuwa awali kwa sababu yeye pia ni mbunifu na alikaa chini akafikiria aje na wazo la tofauti.
"Watu kila siku wanajitokeza wanabuni tisheti, makoti na vitu vingine, mimi nilikaa chini nikafikiria kwanini mama zetu, dada zetu wanaenda kununua nguo za ndani za mtumba Mwenge na kwenye masoko mengine?
Nikaona si kitu kizuri kwa kuwa hizo zimetoka nje ya nchi na zimeshavaliwa kwa hiyo mimi ndo nikaona nibuni nguo za ndani kwa ajili yao".
Msanii huyo anasema kuwa ratiba zake za kutengeneza filamu na muziki zitakapokaa vizuri anataka kurudi shule kumalizia 'Degree' yake ya Masoko ambayo alishaanza lakini alishindwa kuendelea kutokana na kazi.
Hemed ambaye hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wa 'Going Crazy' anasema baada ya wimbo huo anatarajia kuachia video mbili za nyimbo zake mpya ambazo ni 'Far away' aliyomshirikisha Mabeste' na 'Rest of ma life' aliyomshirikisha Mr Blue.

Nafasi Za Kazi -March 15th - 1st April

DRIVER
Qualifications: Holder of  a secondary education exam,Holder of class C driving licence
Apply: The Regional Manager,
Tanzania National Agency
(TANROADS)
Box 30150  Dar es salaam
Details: The Gurdian, March 6 2013
Deadline: March  18, 2013

OFFICE ASSISTANT
Qualifications: Holder of  a secondary education exam.
Apply: The Regional Manager,
Tanzania National Agency
(TANROADS)
Box 30150  Dar es salaam
Details: The Gurdian, March 6 2013
Deadline: March  18, 2013

CASHIER
Qualifications: Minimum holder s of ordinary Diploma in Accounting  or certificate of Accountancy from a recognized institution
Apply: The Regional Manager,
Tanzania National Agency
(TANROADS)
Box 30150  Dar es salaam
Details: The Gurdian, March 6 2013
Deadline: March  18, 2013

PROGRAMME OFFICER,PRIVATE  SECTOR AND CIVIL SOCIETY
Qualifications:A degree in social science discipline
Apply: recruitment@trademarkea.com
Details: The Gurdian, March 6 2013
Deadline: March  29, 2013

PROGRAMME MANAGER
Qualifications:Business Administration,Economics,Development studies,International Trade,Planning,finance ir related field.
Apply: recruitment@trademarkea.com
Details: The Gurdian, March 6 2013
Deadline: March  29, 2013

FINANCE AND ADMINISTRATION OFFICER
Qualifications: Advance diploma in Accounting,B.com-financeApply: The Human resource manager,Elizabeth Glaser pediatric Aids foundation,Box 1628 Dar es salaam
Details: Daily news,
March 4 2013
Deadline: March  15, 2013

CREDIT RISK MANAGER-CONSUMER LOANS
Qualifications: Bachelor degree or Masters degree in Accounting /Banking /finance/Economics/Statistics/Risk management
Apply:Human resources Business partiner-(Retail credit)
National Bank of Commerce
Box  1863 , Dar es Salaam
Details: Daily news ,
March 4, 2013
Deadline: March 16, 2013

IT MANAGER
Qualifications: Bachelor degree in information systems or commensurable experience
Apply: The Human resource manager,Elizabeth Glaser pediatric Aids foundation,Box 1628 Dar es salaam
Details: Daily news, March 4 2013
Deadline: March  15, 2013

MONITORING AND EVALUATION OFFICER,TB/HIV PROJECT.
Qualifications: http://www.path.org
Apply: http://www.path.org
Details: Daily news, March 4 2013
Deadline: March  15, 2013

DISTRICT TUBERCULOSIS/HIV COORDINATOR
Qualifications: http://www.path.org
Apply: http://www.path.org
Details: Daily news, March 4 2013
Deadline: March  15, 2013

MONITORING AND EVALUATION OFFICER,TB/HIV PROJECT.
Qualifications: http://www.path.org
Apply: http://www.path.org
Details: Daily news, March 4 2013
Deadline: March  15, 2013

SECRETARY
Qualifications: Hokder of ordinary secondary education certificate with passes in English and swahili,full secretarial course and computer application skills in windoes ,microsoft office,excel,Access,Power point,internet,e-mail and publusher
Apply:Director General,Tanzania Civil Aviation Authority,
Box  2819, Dar es Salaam
Details: Daily news ,March 4, 2013
Deadline: March  19, 2013

INFORMATION TECHNOLOGY MANAGER
Qualifications: A Bachelor Degree in computer science ,LINUX or CISCO
certification
Apply:Director General,Tanzania Civil Aviation Authority,
Box  2819, Dar es Salaam
Details: Daily news ,March 4, 2013
Deadline: March  19, 2013

FLIGHT OPERATIONS INSPECTOR
Qualifications: An airline transport pilot license (ATPL) with a flying experience of at least 5000 flight hours as a pilot in command
Apply:Director General,Tanzania Civil Aviation Authority,
Box  2819, Dar es Salaam
Details: Daily news ,March 4, 2013
Deadline: March  19, 2013

MOTHERS/AUNT
Qualifications: minimum of four years secondary school education
Apply: The National Director,
SOS Village Tanzania,
Box 80462 Dar es Salaam
national.office@sos-tanzania.org
Details: Mwananchi Febr 25, 2013
Deadline: March  17, 2013

CREDIT RISK MANAGER-SME LOANS
Qualifications: Bachelor degree or Masters degree in Accounting /Banking /finance/Economics/Statistics/Risk management
Apply:Human resources Business partiner-(Retail credit)
National Bank of Commerce
Box  1863 , Dar es Salaam
Details: Daily news ,March 4, 2013
Deadline: March 16, 2013

LEGAL OFFICER
Qualifications: Holder of LLB from a recognized institution
Apply:Managing Editor,Tanzania Standard ( Newspaper) Limited
Box  9033 , Dar es Salaam
Details: Daily news
March 4, 2013
Deadline: March 13, 2013

NATIONAL PROJECT COORDINATOR
Qualifications :Masters degree in public policy,public Administration,Economic Development,Development Studies,law,sociology,International development,or any other relevant field
Apply: https://jobs-undp.org/cj_viewjob.cfm?job_id=35987
Details: Mwananchi ,March  4  2013
Deadline: March  15, 2013

RECEPTIONIST /TELEPHONE OPERATOR
Qualifications :Secondary school education
Apply: https://jobs-undp.org/cj_viewjob.cfm?job_id=35987
Details: Mwananchi ,
March  4  2013
Deadline: March  15, 2013

ADMINISTRATIVE AND FINANCE ASSISTANT
Qualifications :Bachelor or Business Administration in  Accounting /Finance degree or a relevant degree at least CPA 2 or relevant financial /Accounting management qualification.
Apply: The Human resources unit,
World Afroforestry centre (ICRAF) e-mail-icrafhru@cgiar.org
Details: Mwananchi ,
March  5  2013
Deadline: March  18, 2013

CREDITY  RISK  MANAGER - SME LOANS

Qualifications: Bachelor degree Master’s degree in Accounting /Banking/Finance/Economics/Statistics/Risk Management
Apply: The Human Resources
Business Partner
National Bank of Commerce
Box  1863 , Dar es Salaam
Details: The Guardian March 1, 2013
Deadline: March  16, 2013

CREDITY RISK MANAGER - CONSUMER LOANS
Qualifications: Bachelor degree Master degree in Accounting /Banking/Finance/Economics/Statistics/Risk Management
Apply: The Human Resources
Business Partner
National Bank of Commerce
Box  1863 , Dar es Salaam
Details: The Guardian March 1, 2013
Deadline: March  16, 2013

CONSERVANCY MANAGER
Qualifications: Bachelor’s degree in Conservation,Natural Resource Management,Tourism Management or related
Apply: www.awf.org
Details: The Guardian March 1, 2013
Deadline: March  15, 2013

PROGRAMME OFFICER,COMMUNITY DEVELOPMENT
Qualifications: Bachelor’s degree in Community Development Social Sciences or related field
Apply: www.awf.org
Details: The Guardian
March 1, 2013
Deadline: March  15, 2013

MONITORING AND EVALUATION ASSISTANT
Qualifications: A first degree in a Social Sciences -related discipline is desiable and qualitive research experience including familiariy with software an added advantage
Apply: info@uzikwasa.or.tz
Details: The Guardian March 1, 2013
Deadline: March  15, 2013

FREELANCE SALES EXECUTIVES
Qualifications: A level with at least 2 years experience in sales experience preferably in the media industry
,Diploma /degree in sales & Marketing is an added advantage
Apply: Human Resources Department East Africa Television
Box  4374 , Dar es Salaam
Details: The Guardian Febr 28, 2013
Deadline: March  15, 2013

Mamilioni yatolewa kwa dijitali

KATIKA mkakati wa kusambaza mawasiliano ya mfumo mpya  wa dijitali katika mikoa 14 nchini, jumla ya Sh50 milioni zimetolewa na Kampuni ya StarTimes ili kuwezesha kazi hiyo.
Meneja Habari wa StarTime, Erick David aliitaja mikoa ambayo kampuni hiyo imewekeza kuwa ni pamoja na Shinyanga, Iringa, Tabara,  Ruvuma, Mara, Kigoma  na Manyara.
David aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, alisema hatua hiyo ni kuunga mkono Serikali kuhusu dhamira ya kusambaza mfumo  huo nchi nzima, ambapo inakwenda sambamba na kutoa huduma mpya ya kukodisha ving’amuzi kwa wateja.
Mikoa mingine ni Singida,  Kusini Pemba, Kaskazini Pemba na Rukwa, Mtwara na Lindi  na kwamba mikoa 23 inatarajia kupatiwa huduma hiyo kufikia mwisho wa mwaka huu.
“Huduma hii ya kukodisha ving’amuzi ni mpya  kutoka Startimes, kutatua changamoto zinazoikabili dijitali na kwamba mteja anatakiwa kutoa Sh39,000 kama dhamana ya kuchukua king’amuzi na pia mteja anatakiwa kulipa  Sh6,000 kama malipo ya kila mwezi  na itakuwa na chaneli 15 za nyumbani na nyinginezo,” alisema David.
Alisema mteja anaweza kurudisha  na akarudishiwa Sh39,000 aliyotoa kama dhamana baada ya matumizi yake na huduma hiyo inayolenga kuwanufaisha watu wa kipato cha chini kwani licha ya kukodishwa  utapata  channel zaidi ya 15 saa 24 kwa mwezi mzima.
Alisema katika kuifanya jamii kuwa karibu na ulimwengu huu wa dijitali na kuepuka  gharama kubwa za ununuzi wa ving’amuzi na malipo ya vifurushi kwa kila mwezi kampuni yao inarahisisha hilo.

Kifo cha Chavez kuchunguzwa

The Late President Hugo Chavez
Venezuela. Serikali ya Venezuela imesema kuwa ipo mbioni kuanza uchunguzi rasmi ili kuchunguza kwa kina kama ugonjwa wa saratani aliokuwa nao Rais Hugo Chavez umesababishwa na maadui wa kigeni.

Kauli hiyo ilitolewa na aliyekuwa Makamu wa Chavez ambaye kwa sasa aliteuliwa kuwa rais wa muda Nicolas Maduro aliahidi kuanzisha uchunguzi ili kuchunguza madai yaliyotolewa na watu wengi akiwemo Chavez mwenyewe kwamba maradhi yaliyokuwa yakimsumbua hadi kusabisha kifo chake yalitokana na sumu aliyopewa.

Maduro alisema Serikali ya Caracas itawaalika wanasayansi wa nchi za nje kushirikiana na kamati ya nchi hiyo ili kuchunguza tuhuma hizo.
Rais Hugo Chavez wa Venezuela alifariki dunia tarehe 5 mwezi huu baada ya kuuugua saratani kwa muda wa miaka miwili.

Kwa sasa serikali ya nchi hiyo ipo chini ya Nicolas Maduro aliyekuwa makamu wa rais chini ya Rais hugo Chaves licha ya kuwa serikali ilimkabidhi madaraka vyama vya upinzani vilipinga suala hilo kwa madai kuwa lipo kinyume na sheria ya nchi hiyo.

Hugo Rafael Chavez Frias alizaliwa Julai 28, 1954. Alishika madaraka ya kuiongoza Venezuela mwaka 1999. Kufuatia itikadi yake ya kisiasa ya Kibolivarian na “Usoshalisti wa karne ya 21”, amelenga katika kutekeleza mageuzi ya usoshalisti katika nchi kama sehemu ya mradi wa kijamii inayojulikana kama Mapinduzi ya Wabolivia, ambayo yameshuhudia utekelezaji mpya wa katiba, demokrasia shirikishi na kutaifisha viwanda kadhaa muhimu.

TCRA yawavimbia wamiliki wa televisheni nchini

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haitarudi nyuma kwenye suala la kutumia mfumo wa matangazo kupitia njia ya dijitali na kwamba mfumo huo utaendelea kutumika.

Kauli ya TCRA imekuja siku moja baada ya wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini kutishia kusitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi juzi alisema hakuna haja ya kurusha matangazo kwa hasara kwani watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving’amuzi. Licha ya Moat kutoa kauli hiyo juzi, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma alisisitiza kwamba TCRA haiwezi kurudi nyuma katika suala hilo kwani mfumo huo utaendelea kutumika.

Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye warsha ya mambo ya mionzi, alisema wao kama TCRA hawawezi kurudi nyuma katika suala hilo na kwamba msimamo wao wa kuendelea kutumia mfumo wa matangazo kwa njia ya dijitali upo palepale.

“Sikiliza niwaambie waandishi, leo tupo hapa kwa suala moja la mambo ya mionzi, lakini kwa ufupi ni kwamba sisi hatuwezi kurudi nyuma katika suala hilo la mfumo wa dijitali,” alisema Profesa Nkoma.

Alisema ili kuelezea jambo hilo kwa undani watafanya warsha ya kuzungumzia mambo hayo na kwamba hapo kila kitu kitaelezwa kwa kina.

“Tutafanya warsha kueleza mambo hayo yote na nyie pia kama waandishi mtaelezwa kila kitu, lakini kwa sasa naomba tuyaache kama yalivyo,” alisema.

TCRA ilizima mitambo ya analojia na kuhamia dijitali, Desemba 31, mwaka jana kitendo ambacho Moat wanadai kimepunguza mapato yanayotokana na matangazo.

Mkuu wa Usalama Chadema akamatwa

Lwakatare

Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Chadema,Wilfred Lwakatare jana alikamatwa, akahojiwa na kupekuliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi wa uvunjifu wa amani.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso aliliambia Mwananchi jana kuwa Lwakatare alikamatwa kutokana na taarifa zilizopatikana kutoka katika video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwahamasisha watu kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani au uhalifu. Alipoulizwa mahali na lini alikamatwa Lwakatare, Senso alisema hilo halijalishi, lakini jambo la msingi ni kwamba wako naye kwa ajili ya uchunguzi na hakutaka kuweka bayana ni lini wangemwachia.

Siku nzima ya jana mitandao ilikuwa imetawaliwa na habari ya picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky. Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu, ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.

Alionyeshwa akiwataka watu hao kumkamata bila ya kumdhuru Msacky, lakini wamtupe mbali kama njia ya kumnyamazisha. Alikuwa anamtuhumu Msacky kama alikuwa anashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ili kukihujumu chama chao.

“Inabidi mfahamu nyendo za mtu huyu, kama anapenda vitu kama kutembea usiku au kinywaji anachokunywa,” alinukuliwa kwenye mtandao huo.

Pia anaonekana kwenye video hiyo akitoa mbinu mbalimbali za namna ya kufanya utekaji nyara.

Wakili wa Lwakatare alonga
Wakati akihojiwa na kupekuliwa, Lwakatare aliongozana na wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, ambaye alilieleza Mwananchi kuwa mteja wake alichukuliwa kutoka ofisini kwake kwenye Makao Makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kicheere alidai kuwa hakuwa na uhakika kuwa Lwakatare alikamatwa muda gani ofisini kwake kwani yeye aliitwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi saa 9.00 alasiri.Mwananchi, hata hivyo, lina taarifa kuwa Lwakatare alikamatwa na askari wanne saa 7.00 mchana na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi.

Lwakatare, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipokamatwa alifuatana na maofisa kadhaa wa Chadema akiwamo Ofisa wa Ulinzi wa chama hicho, Hemed Sabula na Ofisa wa Mawasiliano aliyejulikana kwa jina moja tu la Karungebe.

Alichukuliwa ndani ya gari aina ya Land Cruiser na kupelekwa moja kwa moja Makao Makuu ya Jeshi la Polisi katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Mahojiano
Kicheere alisema Lwakatare alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi ingawa alidai polisi hawakubainisha ni uchochezi upi.
Mahojiano hayo kwa Lwakatare yaliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Obadia Jonas.
“Lwakatare alihojiwa kuanzia saa 9.00 alasiri hadi 9.55 jioni na tuhuma zilizomkabili ni uchochezi. Ila askari hawakuniambia ni uchochezi upi,” alieleza Kicheere. Alisema kuwa baada ya mahojiano yale waliamriwa kwenda nyumbani kwa Lwakatare kwa ajili ya upekuzi.

Upekuzi
Lwakatare, ambaye anaishi eneo la Kimara King’ong’o jijini Dar es Salaam, alisindikizwa na askari saba walioongozwa na ACP Jonas. Katika msafara huo wa kwenda kupekua nyumbani kwake, maofisa wa Chadema walizuiwa kuongozana naye, isipokuwa mwanasheria wake, Kicheere, ndiye aliruhusiwa kuongozana naye.

“Tunavyoongea na wewe hivi sasa ni kwamba upekuzi unaendelea katika vyumba vya nyumba . Kwa sasa tuko ndani ya chumba chake cha kulala,” alieleza Kicheere.

Kicheere alisema upekuzi huo ulianza saa 10.30 jioni na ulilenga katika kutafuta nyaraka ambazo zingeweza kutumika kama ushahidi wa tuhuma hizo. Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa upekuzi kilichokuwa kinatakiwa kufuata ni kuandikisha maelezo katika Kituo cha Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

“Hawa jamaa wanaendelea na upekuzi na hawajapata kitu chochote muda huu tunavyoongea na wewe. Ila tukimaliza tutarudi Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuandikisha maelezo,” aliongeza Kicheere.

Dk Slaa anena
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema polisi walifika katika ofisi za chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuomba kuzungumza na Lwakatare.

Tume ya Mizengo Pinda yaanza kuhoji wanafunzi, walimu

Mh Pinda
Dar es Salaam. Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012, imeanza kazi kwa kuwahoji walimu, wanafunzi na wajumbe wa bodi za shule kuhusu sababu za matokeo mabaya.
Mwenyekiti wa tume hiyo Profesa Sifuni Mchome, alisema jana kwamba shughuli hiyo imeanza katika Kanda ya Dar es Salaam ambapo wajumbe watatembelea shule 12.

“Tumeamua kuzungumza na wanafunzi waliopo shuleni na wale waliofanya mtihani huo watakaopatikana ili kujua ni nini kilichofanya wakapata alama hizo, pia itakuwa njia rahisi ya kupata watu wengi ikiwa ni pamoja na bodi za shule,” alisema Profesa Mchome:
“Kazi kwa Dar es Salaam ilianza Jumatatu na itaisha Ijumaa, kuna shule ambazo zimeainishwa. Tukifika kwenye hizo shule na kama zipo shule zingine jirani tutawaita waje kutoa maoni yao.” alisema.

Profesa Mchome alisema kuwa, ili kufanikisha shughuli hiyo wameteua kanda tano ikiwamo ya Dar es Salaam, Kusini, Mashariki, Kati na Kanda ya Magharibi ambayo itahusisha Mikoa ya Geita na Simiyu.

Profesa Mchome alieleza kuwa, ili kupata maoni ya wananchi wengi wamefungua tovuti inayoitwa www.tumek4.go.tz ili wengine watoe maoni huko.

Alisema kuwa, kanda hizo zimetengwa kwa kuzingatia hadidu za rejea zilizotolewa na Waziri Mkuu, ambapo wamechangua shule zilizofanya vibaya, zilizokuwa na ufaulu wa kati na zilizofanya vizuri ambazo ni zile za Serikali na zisizo za Serikali.

Alisema kuwa, tayari wameshazungumza na maofisa elimu pamoja na Muungano wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahosa).

Alisema kuwa, baada ya kutembelea shule hizo Dar es Salaam, juma lijalo timu hiyo itaenda katika kanda nyingine ambapo zitatembelewa shule 13.

Alisema kuwa, leo ratiba ya shughuli ya tume hiyo itawekwa katika tovuti yao.Profesa mchimo aliwataka wananchi watoe zaidi maoni yao kupitia tovuti hiyo, pamoja na vyombo vya habari ili waweze kukamilisha shughuli hiyo kwa kupata maoni ya watu wengi.

Papa mpya apatikana, achagua jina la Francis I


Kardinali Jorge Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuongoza Kanisa Katoliki Duniani, akiwa ni wa kwanza kutoka barani Amerika na wa kwanza kutoka nje ya Ulaya kwa zaidi ya miaka 1,000.
Baada ya kuchaguliwa na makardinali wenzake 115, Kardinali Jorge Bergoglio (76) alichagua kufahamika kwa jina la Francis I.
Maelfu ya mahujaji, watalii na waumini wa Kanisa Katoliki waliokuwa wamejazana katika Viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Petro, Vatican kushuhudia moshi mweupe uliofuka saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kuashiria kuchaguliwa kwake, waliripuka kwa shangwe, nderemo na vifijo.
Muda mfupi baada ya moshi huo kutoka, kardinali mmoja alisimama katika ‘varanda’ ya Kanisa la Mtakatifu Petro na kutangaza “Habemus Papum” (tumepata papa mpya).
Papa Francis I alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanawania nafasi hiyo na papa anayeondoka, Benedict XVI mwaka 2005, ambapo aliripotiwa kuibuka wa pili.
Kabla ya kuchaguliwa kwake, Papa Francis I ambaye kwa wadhifa wake pia anakwenda kuwa Askofu wa Roma, alikuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires, Argentine na kwa muda wote wa utumishi wa utumishi alikuwa huko huko nyumbani.
Anakuwa Papa wa 266 kuwahi kuongoza kanisa hilo lenye waumini zaidi ya bilioni 1.2 duniani.
Baada ya kutangazwa kwake, Papa Francis I alijitokeza kuzungumza  kwa mara ya kwanza kama Askofu wa Roma.
Akiwa amechaguliwa katika awamu ya tano ya upigaji kura, inaelezwa kuwa alikuwa miongoni mwa mapapa waliochaguliwa kwa haraka baada ya muda mrefu, akiwa sawa na Benedict XVI (2005) na Pius XII aliyechaguliwa mwaka 1939.
Mshindi alitakiwa kupata kuta 77 au robo tatu ya makardinali 115 walioshiriki uchaguzi huo.
Papa Francis I anachukua nafasi iliyoachwa na Papa Benedict XVI aliyejiuzulu Februari 28, mwaka huu, ikiwa  ni miaka 600 tangu Papa wa mwisho kujiuzulu.
Yeye ni nani
Papa Francis I, ni Papa wa kwanza kutoka Shirika la Jesuit ambaye ametumia muda wake mwingi wa utumishi nyumbani Argentina.
Anafahamika kwa utumishi uliotukuka kwa uangalizi wa kanisa na mapadri, mambo ambayo yanatajwa kuwa sifa kubwa ya kuchaguliwa kuwa Papa.
Papa huyo amedumu katika maisha ya kufundisha na kuongoza mapadri. Amefanya kazi Amerika ya Kusini ambako kuna Wakatoliki wengi. Kardinali Bergoglio anatambulika kwa kutamadunisha Kanisa la Argentina, lililokuwa miongoni mwa makanisa ya kihafidhina huko Amerika Kusini.
Amechagua jina la Papa Francis I, chini ya uangalizi wa Mtakatifu Francis wa Assisi.
Alizaliwa Buenos Aires katika familia ya mfanyakazi wa reli. Alipata upadrisho mwaka 1969.
Aprili 15, 2005, mwanasheria wa haki za binadamu alimfungulia mashtaka ya jinai  kwa kushirikiana na maofisa wa jeshi kuwateka mapadri wawili wa Jesuit mwaka 1976, akiwa kiongozi wao aliwafukuza katika utumishi kutokana na migogoro katika jumuiya hiyo.

Rais wa Venezuela Hugo Chavezi afariki

Wednesday, March 6, 2013




Amefariki akiwa na umri wa miaka 58, Makamu wa Rais Nicola Maduro amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Awali ilielezwa kuwa Rais Chavez alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kansa

Kwa habari zaidi ungana nasi baadaye