Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki na filamu pia Hemed Seif Suleiman aka PHD, amesema kuwa mwaka huu hatoigiza sana kwenye filamu za watu kwasababu ameingia mkataba na kampuni moja ya usambazaji ambayo inamtaka kutengeneza filamu zake mwenyewe 7 kwa mwaka.
Hemed alisema kuwa mkataba huo utamfanya yeye kufikiria zaidi filamu zake kuliko kucheza kwenye filamu za watu wengine.
Hemed alieleza kuwa ubize huo wa mwaka pia ndo
unamfanya kushindwa kuanza kutengeneza nguo za ndani za wanawake kama
alivyosema mwaka huu kuwa anatarajia kuanza kubuni nguo zake za kike za
ndani za wanawake.
Alisema kuwa bado mipango ya nguo hizo iko
palepale kama ilivyokuwa awali kwa sababu yeye pia ni mbunifu na alikaa
chini akafikiria aje na wazo la tofauti.
"Watu kila siku wanajitokeza wanabuni tisheti,
makoti na vitu vingine, mimi nilikaa chini nikafikiria kwanini mama
zetu, dada zetu wanaenda kununua nguo za ndani za mtumba Mwenge na
kwenye masoko mengine?
Nikaona si kitu kizuri kwa kuwa hizo zimetoka nje
ya nchi na zimeshavaliwa kwa hiyo mimi ndo nikaona nibuni nguo za ndani
kwa ajili yao".
Msanii huyo anasema kuwa ratiba zake za
kutengeneza filamu na muziki zitakapokaa vizuri anataka kurudi shule
kumalizia 'Degree' yake ya Masoko ambayo alishaanza lakini alishindwa
kuendelea kutokana na kazi.
Hemed ambaye hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wa
'Going Crazy' anasema baada ya wimbo huo anatarajia kuachia video mbili
za nyimbo zake mpya ambazo ni 'Far away' aliyomshirikisha Mabeste' na
'Rest of ma life' aliyomshirikisha Mr Blue.


I’m a Freelance Web Designer & Developer. I’m an enthusiastic, creative designer and geek with 3 years of strong commercial experience and a passion for creating beautiful, accessible websites using Web Standards
No comments:
Post a Comment
Tuachie Ujumbe wako hapa .