Sitta alaumu mawaziri kwa kugeuzwa chambo

Wednesday, March 20, 2013

Mh Samwel Sitta

 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema idadi ndogo ya walipa kodi nchini inachangiwa na  baadhi ya mawaziri kutumika kama chambo cha ukwepaji walipa kodi.         
Akizungumza kwenye Siku ya Ustawi wa Jamii jana, Sitta alisema  Tanzania ina watu milioni 45, lakini walipa kodi ni milioni moja.
Alisema wengi hukwepa kwa kutumia mianya ya viongozi waliopo madarakani, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya nchi.
Pia, Sitta alisema suala la kujuana na uongozi wenye ulafi na ubinafsi, unaonekana kuchangia kwa  kiasi kikubwa suala la umaskini kuendelea kuitesa nchi.
Alisema hali hiyo inasababisha tabaka moja la viongozi kufaidi keki ya Watanzania, huku idadi kubwa ya wananchi wakisalia kuogelea kwenye dimbwi la umaskini. Waziri Sitta alisema viongozi walafi na waotumia vyeo vibaya kufuja mali za umma, hutoa mfano mbaya  kwa watendaji wengine wanaohudumia watu wenye mahitaji.
Alisema chanzo cha matatizo mengi ya watoto, umaskini, ukosefu wa usawa na mengine ni matokeo ya uchumi mdogo.

No comments:

Post a Comment

Tuachie Ujumbe wako hapa .