Mvua kubwa iliyonyesha jana jijini Dar es Salaam, ilisababisha mafuriko makubwa katika baadhi ya maeneo, hivyo nyumba kadhaa kujaa maji na baadhi ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.
Mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua iliyoanza
kunyesha muda wa asubuhi, pia yalisababisha hasara kubwa kutokana na
vitu na mali mbalimbali kusombwa na maji.
Mwananchi lilitembelea maeneo mbalimbali na
kushuhudia wananchi wakihangaika kuokoa mali zao, baada ya nyumba
walizokuwa wakiishi kujaa maji.
Barabara kadhaa zilikuwa hazipitiki kutokana na
kujaa maji, huku baadhi ya nguzo za umeme na simu ambazo zilikuwa karibu
na mifereji ziliharibiwa na kusombwa na maji.
Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
walionekana katika maeneo kadhaa ya jiji wakihangaika kuokoa baadhi ya
nguzo hizo.
Athari kubwa ya mafuriko hayo ilitokea katika eneo
la Kigogo Darajani ambako baadhi ya nyumba zilikuwa zimejaa maji na
baadhi ya vitu vilionekana vikielea kwenye mikondo mikubwa ya maji.
Mmoja wa waathirika hao, Andrew Simon (35) alisema
nyumba yake ilijaa maji kwa takriban futi nne kwenda juu na kusababisha
hasara ya mali ambayo alikuwa bado hajafahamu thamani yake.
“Sisi tulitoka kwenda kwenye shughuli zetu,
baadaye tulipigiwa simu kwamba kuna mafuriko jambo lililonifanya nirudi
haraka ndiyo nikakuta nyumba yetu ikiwa imefurika, huku vyombo vyote
vikiwa vimeharibika,” alisema Simon.
Kuhusu kutii agizo la Serikali la kuwataka
wananchi wa mabondeni kuyahama makazi yao, Simon alisema yeye ni
mpangaji hakufahamu kuwa mafuriko yangetokea.
Mbali na Kigogo Darajani maeneo mengine ya Ubungo,
Tabata, Magomeni Kagera, Jangwani, Msasani, Mikocheni, Kimara na Mbezi
pia yaliathiriwa na mvua hizo hali iliyozua hofu miongoni mwa wakazi wa
maeneo hayo.
Pia hali ilikuwa mbaya eneo la Tabata Relini
nyumba na magari vilifunikwa na maji na kuwafanya watu kupanda kwenye
mapaa ya nyumba zao.
Reli inayopita katika eneo hilo ilifunikwa na maji
kiasi cha kusababisha kuwapo kwa wasiwasi kama treni ya usafiri wa
abiria itafanya kazi leo.


I’m a Freelance Web Designer & Developer. I’m an enthusiastic, creative designer and geek with 3 years of strong commercial experience and a passion for creating beautiful, accessible websites using Web Standards
No comments:
Post a Comment
Tuachie Ujumbe wako hapa .