Nafasi za kazi, Endless Fame

Wednesday, February 27, 2013




Kampuni ya Endless Fame ya Wema Sepetu,imetanga nafasi za kazi mbalimbali kama inavyoonyesha kwenye tangazo lao hapo chini.


NMB yapata Tuzo ya Superbrand

NMB imepata tuzo ya Superbrand baada ya kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na huduma za masoko, mtandao mkubwa wa matawi ambapo imeweza kufikia wateja 800,000 nchi nzima. Pia imeweza kutoa huduma mbadala kama Internet Banking, kituo cha huduma kwa wateja na POS.




Mkuu wa masoko NMB Imani Kajula akipokea tuzo toka kwa Mkurugenzi wa Superbrand East Africa- Jawad Jaffer.



Wafanyakazi wa NMB wakifurahia tuzo ya Superbrand

M-Pesa yapata tuzo ya Superbrand



NEMBO ya huduma ya kuweka, kutoa fedha, kununua na kulipia ankara (M-Pesa) kwa bidhaa mbalimbali kupitia simu ya mikononi ya Vodacom ya nchini, imeibuka mshindi kwenye tuzo za ubora wa huduma na viwango za kimataifa za Super Brands kwa mwaka 2013/14.

Akizungumzia tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Rene Meza, alisema kuwa ni jambo la kujivunia kwa kampuni yake kufanikiwa kupata tuzo hiyo kubwa na yenye heshima kitaifa na kimataifa.

“Tunawashukuru Watanzania kwa kuendelea kuiunga mkono, kuiamini, kuipokea na kuitumia maradufu huduma ya M-Pesa,” alisema Meza.

TCRA yafunga Radio station 2, Clouds FM yapewa onyo kali

Tuesday, February 26, 2013

KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.

Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa
kufanya.

Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.

Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

RAIS KIKWETE AWASILI NCHINI ETHIOPIA KUHUDHURIA UTIWAJI SAINI MPANGO WA UMOJA WA MATAIFA WA AMANI, USALAMA NA USHIRIKIANO KATIKA DRC

Monday, February 25, 2013






TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 23, 2013 kuhudhuria utiwaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mpango huo unatarajiwa kutiwa saini kesho Februari 24, 2013 na Wakuu wa Nchi kutoka Ukanda wa Maziwa Makuu, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Angola, Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kongo (Brazaville), Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya Afrika Kusini.
Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki Moon, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma, pamoja na wenyeviti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) watatia saini Mpango huo kama mashahidi na wadhamini.
Mpango huo una nia ya kuchangia juhudi ambazo zimefanywa na Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) katika kutafuta amani Mashariki ya Kongo na ukanda wote wa Maziwa Makuu kwa ujumla.
Mpango huo pia umetilia maanani mapendekezo muhimu yaliyokubalika baada ya mashauriano kati ya wakuu wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
IMETOLEWA NA:
MUHIDIN ISSA MICHUZI,
MWANDISHI WA HABARI WA RAIS, MSAIDIZI,
IKULU,
DAR ES SALAAM.
23 FEBRUARI, 2013

MECHI YA YANGA, AZAM YAINGIZA MIL 240/-

Mechi namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.
Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 6,975,669.36.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Matokeo Kidato cha Nne 2012 ni FEKI (yamepikwa) - GREEN ACRES

Friday, February 22, 2013

Mkurugenzi Green Acres afichua siri nzito


WAKATI mjadala wa matokeo mabaya ya kidato cha nne ukiendelea kulitikisa taifa, kashfa mpya ya matokeo hayo imeibuliwa.

Kashfa hiyo mpya imeibuliwa na Mkurugenzi wa Shule ya Green Acres, Julian Bujugo, kwamba matokeo ya baadhi ya shule nchini ikiwamo yake yamechakachuliwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Bujugo alisema kuwa baadhi ya wanafunzi kwenye shule yake hawakufanya mitihani ya kidato cha nne, lakini matokeo yanaonesha wamefaulu kwa kupata alama za juu.

Alitaja mfano wa mwanafunzi, Humphrey Sanga, mwenye namba 01197/148, ambaye hakufanya mitihani hiyo lakini matokeo yanaonesha amefaulu kwa kupata alama nzuri.

“Huyu mwanafunzi tulimsimamisha na hakufanya mitihani, lakini matokeo yake yanaonekana amepata hivi; Civics D, Historia D, Jiografia C, Kiswahili D, English C, Physics D, Chemistry C, Biology C, Basic Mathematics D, ambapo amepata daraja la tatu pointi 24,” alisema Bujugo.

Alimtaja mwanafunzi mwingine, Martin Rushaigwa, namba 01197/0173, ambaye alifanya masomo ya ‘Arts’.
Alisema matokeo ya mwanafunzi huyo yanaonesha kuwa ameongezewa alama za masomo ya biashara ya Bookeeping na Commerce, ambayo hakuyafanya kabisa.

Alimtaja mwanafunzi mwingine aliyefanya mtihani huo lakini matokeo yake yanaonesha amewekewa ‘absent’ na mwanafunzi mwingine, Mbazi Volta, hakufanya mitihani lakini amepewa alama za ufaulu.

“Matokeo hayo yananipa wasiwasi kwamba yanaweza kuwa yamechakachuliwa,” alisema Bujugo.

Mkurugenzi huyo anaiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudia kusahihisha mitihani hiyo ili kuondoa ukungu ulioligubika taifa kwa sasa kuhusu matokeo ya kidato cha nne.

“Naomba usahihishaji urudiwe, maana huu ni ubabaishaji mkubwa…matokeo hayo yamewaathiri watoto kisaikolojia na sijui watakwenda wapi?,” alihoji.

Alisisitiza kuwa usahihishaji urudiwe kwani katika shule hiyo wanafunzi wenye uwezo mkubwa tangu walipoanza kidato cha kwanza ndio waliofanya vibaya wakati waliokuwa wakifanya vibaya, wameibuka na alama za juu.

Mkurugenzi huyo alisema wazazi wa watoto hao wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii kujadiliana kuhusu matokeo hayo na hatua za kuchukua.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Msemaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), John Nchimbi, alisema si kweli kuwa matokeo hayo yamechakachuliwa bali ni matokeo halisi ya shule hiyo.

Alisema iwapo mkurugenzi wa shule hiyo ana shaka na matokeo hayo, alitakiwa kufika katika ofisi za baraza hilo ili apatiwe taarifa sahihi kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari.

“Mi nimeangalia hayo majina, naona yapo sawa na hata huyo mwanafunzi ambaye anasemekana hakufanya mitihani na akapewa alama…napenda kusema kuwa alama alizopewa si zake na hata katika orodha yetu anaonekana kuwa hakufanya mitihani,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa na wenzake, wamekuwa bubu kueleza endapo wako tayari kujiuzulu au la.

Tanzania Daima ilifika wizarani hapo jana kutaka kuonana na Waziri Kawambwa ili atoe msimamo wake, mwandishi alijibiwa kuwa waziri huyo alikuwa kikaoni na asingeweza kutoka.

Hata waziri alipopigiwa simu pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo naye hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa alikuwa kikaoni.

Naye Naibu Waziri, Philipo Mulugo, alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kueleza msimamo wake, simu yake iliita bila kupokewa na hata hakuwa tayari kujibu meseji ya ujumbe mfupi.

Makada wa CCM wamng’ang’ania Lema

Friday, February 15, 2013

MAKADA watatu wa CCM mkoani Arusha wameendelea kumng’ang’ania Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema baada ya kuwasilisha Mahakama ya Rufani maombi ya marejeo ya hukumu iliyomrudisha bungeni mbunge huyo.


Lema alivuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, 2012 kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.


Hata hivyo, Mahakama ya Rufani ilimrejesha bungeni Lema baada ya kushinda rufaa yake aliyokata mahakamani hapo akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Makada hao wa CCM hawakuridhika na hukumu hiyo na sasa wamewasilisha maombi mahakamani hapo, wakiomba mahakama hiyo ifanye marejeo ya hukumu hiyo huku wakianisha hoja kadhaa za kupinga hukumu hiyo.


Katika hukumu yake, iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Elizabeth Mkwizu, Desemba 21, 2012, Mahakama ya Rufani ilitengua hukumu ya Mahakama Kuu na ikamthibitisha rasmi Lema kuwa ni mbunge halali wa Arusha Mjini.


Katika hukumu hiyo iliyoandikwa na Jaji Bernard Luanda kwa niaba ya jopo la majaji wenzake wawili waliokuwa wakisikiliza rufaa hiyo, Mahakama ya Rufani ilisema kuwa warufani hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi dhidi ya Lema kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi.


“Rufaa imefanikiwa na tunatengua hukumu, tuzo na amri ya Mahakama Kuu.Tunamtangaza mrufani kuwa Mbunge wa Arusha Mjini,” ilisema Mahakama ya Rufani katika hukumu yake hiyo na kuwaamuru wajibu rufaa kulipa gharama za rufaa hiyo.


Hata hivyo, makada hao katika maombi yao hayo wanaliomba jopo la majaji hao lifanye marejeo ya hukumu yake hiyo ama mahakama kupitia kwa jopo jipya la majaji isikilize upya rufaa hiyo na kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ya Lema.


Sambamba na rufaa hiyo, pia makada hao wa CCM wanaomba rufaa yao waliyokata pia wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu Arusha (Cross Appeal), ishughulikiwe haraka.
Katika maombi hayo, makada hao kupitia kwa wakili wao Alute Mughwai wanadai kuwa sababu zilitolewa na jopo hilo la majaji kuhusiana na haki yao ya kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi inapingana na uamuzi mwingine wa mahakama hiyo.


Wanabainisha mkinzano huo kuwa ni katika aina ya sheria ambayo inapaswa kutumika, ambayo ni ya Sheria za nchi za Jumuiya ya Madola na Sheria ya Uchaguzi ya Taifa, huku wakibainisha kuwa mkinzano huo katika suala moja unaharibu hadhi ya mahakama.
Pia wanadai mahakama ilikosea iliposema kuwa hapakuwa na ushahidi katika kumbukumbu za mahakama kuonyesha kuwa wao walikuwa ni wapigakura waliojiandikisha.


Wanaongeza kuwa pia mahakama hiyo ilikosea kusema kuwa haki ya mpigakura katika kupinga matokeo ya uchaguzi yana mpaka na kwamba ni kwa jambo ambalo linahusiana na uvunjwaji wa haki zao za kupiga kura tu.


Katika rufaa yake, Lema kupitia kwa mawakili wake, aliwasilisha hoja 18 za kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, lakini katika uamuzi wake, Mahakama ya Rufaa iliibua na kutolea uamuzi hoja mpya ambayo haikuwa imetolewa na upande wowote

Contact us

Thursday, February 14, 2013

If you seek help, having any comments regarding our posts please do not hesitate to contact us :




Marafiki Village Blog

Email: solo6k@gmail.com


If you think you are able to be a part of our village, please send us your email.


we are looking for volunteers to participate on the growth of our community.