Rais Chavez bado hoi kitandani
Monday, January 21, 2013
RAIS wa Venezuela Hugo Chavez anasemekana kuwa katika hali mbaya kutokana na matatizo yaliyotokana na upasuaji wa kumtibu saratani, ambao alifanyiwa nchini Cuba mwezi Desemba.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 58 anaendelea kupata nafuu katika hospitali moja mjini Havan na hajaonekana hadharani tangu alipofanyiwa upasuaji, ambao ni wa nne katika muda wa miezi 18.
Chavez anatarajiwa kuapishwa kuchukua muhula mwingine wa uongozi wa miaka 6 baada ya kushinda uchaguzi mwezi Oktoba mwaka jana.
Upinzani unataka aondoke madarakani kwa muda ikiwa ugonjwa wake utamzuia kula kiapo, kama inavyosema katiba ya nchi hiyo. Spika mpya wa Bunge la Venezuela Diosdado Cabello na makamu wa Rais Nicolas Maduro walisema wanaendelea kusimama pamoja na Rais Chavez. Hata hivyo inadaiwa kwamba kuapishwa rasmi kwa Rais Hugo Chavez wa Venezuela kwa kipindi kingine kipya cha miaka sita madarakani hapo tarehe 10 Januari kunaweza kuahirishwa iwapo kiongozi huyo anayetibiwa Cuba atashindwa kuhudhuria hafla hiyo. Makamu wa Rais Nicolas Maduro alisema kwamba Serikali ya Venezuela inapanga kuchelewesha hafla hiyo ya kumwapisha wakati ikijaribu kuepuka kumtangaza mtu wa kuchukua nafasi yake au kuitisha uchaguzi mpya katika nchi hiyo ya Amerika ya Kusini Mwanachama wa Nchi Zinazosafirisha kwa Wingi Mafuta Duniani (Opec).
Kiongozi huyo wa Kisoshalisti mwenye umri wa miaka 58 ambaye amekuwa madarakani tokea mwaka 1999 hajaonekana hadharani kwa zaidi ya wiki tatu sasa. Washirika wake wanasema yuko katika hali mbaya kutokana na operesheni ya nne katika kipindi cha miaka miwili kwa saratani iliyoko kwenye fupa lake la nyonga ambayo aina yake haikutajwa.
Upinzani wa kisiasa nchini Venezuela unasema kwamba kuendelea kwa Chavez kuwepo Cuba hapo tarehe 10 mwezi wa Januari ambapo inatajwa kuwa yu mahututi ni sawa na kujiuzulu kwa Rais huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

I’m a Freelance Web Designer & Developer. I’m an enthusiastic, creative designer and geek with 3 years of strong commercial experience and a passion for creating beautiful, accessible websites using Web Standards
No comments:
Post a Comment
Tuachie Ujumbe wako hapa .