Mwakalebela amvaa Bayi TOC
Monday, January 21, 2013
KATIBU Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela amejitokeza kuwania nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).
Mwakalebela alichukua fomu hiyo jana asubuhi na kuijaza na kuirudisha muda huohuo ili aweze kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho uchaguzi wake umepangwa kufanyika Desemba 8, mjini Dodoma.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kurejesha fomu hizo, Mwakalebela alisema,"Kuna wadau wamenifuata na kuniomba nigombee, nimejitathmini na nimeona ninatosha hivyo nimeamua kula sahani moja na Bayi," alisema Mwakalebela.
Alisema,"Ninajiamini na nimejipanga vya kutosha, najua Bayi ni kama Mbuyu TOC na mimi naingia kwa mara ya kwanza, nina wakati mgumu, lakini naamini mambo yatakwenda vizuri," alisema Mwakalebela ambaye amerejea jijini juzi akitokea Dodoma alipokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa CCM.
Mbali na Mwakalebela pia mwanariadha wa zamani Seleman Nyambui naye ametajwa kuwania nafasi ya Ujumbe ndani ya kamati hiyo.
Hadi juzi jioni nafasi ya Katibu Mkuu ilikuwa na mgombea mmoja ambaye ni Filbert Bayi anayetetea nafasi yake na Rais wa TOC, Ghulam Rashid anayetetea pia nafasi yake hiyo.
Wengine waliojitosa na nafasi zao kwenye mabano ni Hamis Abdul (Rais), Henry Tandau ambaye anawania nafasi ya Makamu wa Rais.
Tandau pia alikuwa Mjumbe wa TOC na mkufunzi wa michezo nchini ambaye atachuana na Hassan Jarufu.
Wengine waliojitokeza ni Jamali Idd (Katibu Msaidizi), Charles Nyange, Juma Hamis (Mweka Hazina Mkuu), wakati nafasi ya Mweka Hazina msaidizi inawaniwa na wagombea 16 ambao ni Irene Mwasanga, Linah Kessy, Nasra Juma, Mharami Mchume, Salum Salum, Noolain Sharif, Peter Mwita, Zakaria Gwandu, Suleiman Jabir, Hemedy Hamis, Suleiman Hemed, Abdulrahman Hassan, Salum Hemed, Alen Alex, Haudy Face na Hamis Gulam.
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu katika kamati hiyo lilifikia tamati jana saa 10 jioni wakati uchaguzi mkuu utafanyika Desemba 8 mwaka huu mjini Dodoma.
Wagombea wote watashiriki kwenye usaili utakaofanyika Jumanne ijayo jijini Dar es Salaam na wale watakaopita ndiyo watapata fursa ya kuchuana kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Desemba 8, mjini Dodoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


I’m a Freelance Web Designer & Developer. I’m an enthusiastic, creative designer and geek with 3 years of strong commercial experience and a passion for creating beautiful, accessible websites using Web Standards
No comments:
Post a Comment
Tuachie Ujumbe wako hapa .