TAMASHA LA IDD MOSI DAR LIVE

Wednesday, August 7, 2013

Meneja wa Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu burudani mbalimbali zitakazokuwepo Dar Live sikukuu ya Idd Mosi
WASANII wa muziki watakaopanda katika jukwaa la kisasa la Dar Live sikukuu ya Idd Mosi pamoja na mabondia  wamelonga na wanahabari kwenye mkutano  ambao umefanyika katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo wasanii wametambiana kila mmoja akitamba kuwa atamfunika mwenzake. Vilevile mabondia nao wametunishiana misuli hali inayoonyesha kuwa kutakuwa na bonge la burudani katika sikukuu hiyo ya Idd Mosi.
Katika sikukuu hiyo wasanii Ali Kiba, H-Baba, Chegge, Temba, Dogo Aslay, Bi. Cheka na Bendi ya Mapacha Watatu watashusha bonge la burudani na kuwapa raha mashabiki watakaohudhuria shoo hiyo. Kwa Upande wa masumbwi bondia Francis Miyeyusho atazipiga na Darius Lupupa kutoka nchini Zambia, Chupaki Chipindi atapigana na Ramadhan Kido. Vilevile mabondia wa kike Ester Kimbe na Irene Kimaro wataonyeshana moto siku hiyo.
(PICHA: SHAKOOR JONGO /GPL)

No comments:

Post a Comment

Tuachie Ujumbe wako hapa .