BENKI YA KCB YATOA MISAADA

Wednesday, August 7, 2013

 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB, Godfrey Ndalahwa,akimkabidhi moja ya boksi lenye vifaa vya kumwekea mgonjwa gesi,Mkuu wa Bima ya Afya wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala, Dk.Merina Nkullua, vilivyotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam jana. Katikatini Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya KCB, ChristinaManyenye


HOTUBA YA MKUU WA MASOKO NA MAWASILIANO - BENKI YA KCB TANZANIA, NDUGU CHRISTINA MANYENYE KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI MISAADA YENYE THAMANI YA SHILINGI 7,200,000 KWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA - TAREHE 6 AUGUST, 2013

Dr. Sophinias H. Ngonyani, Mganga Mkuu – Hospitali ya Mwananyamala
Dr. Merina Nkullua – Mganga mkuu wa kitengo cha bima ya afya hospitali ya Mwananyamala
Dr. Izhaka Kimaro Supportive Manager – Hospitali ya Mwananyamala
Wafanyakazi wa KCB Bank,
Waandishi wa habari,
Mabibi na mabwana.
Habari ya asubuhi!
Kwa niaba ya KCB Bank Tanzania, ninayo furaha kuwepo na nyinyi hapa asubuhi ya leo kwa dhumuni la kukabidhi vifaa vya hospitali ambavyo ni oxygen flow meters venye thamani ya Tsh. 7,200,000/= kwa uongozi wa hospitali ya Mwananyamala
Huu ni mwaka wa pili mfululizo ambako benki ya KCB inatoa misaada kwa hospitali ya Mwananyamala. Mwaka jana tulitoa vitanda 65 vikiwemo 60 na loka zake kwa ajili ya wadi ya kinamama na vitano kwa ajili ya kujifungulia (delivery beds) vyote kwa ujumla vikiwa na thamani ya Sh. 45,000,000. Ni matumaini yetu vitanda hivi bado viko katika hali nzuri na hivi karibuni tutafanya ukaguzi wa vitanda hivi ili tufahamu hali halisi na wakinamama wangapi wamefaidika hadi sasa hivi ili tuweze kuona tuwasaidie vipi zaidi.
Hii ni kawaida ya KCB bank kutembelea vituo vyote ambavyo imepeleka misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kuona manufaa yanayotokana na msaada husika. Ni matunzo na matumizi mazuri ya vifaa vinavyotolewa, yatakayoifanya benki ya KCB iongeze msaada au misaada kituo chochote kilichokwishasaidiwa, vivyo hivyo itakua hospitali ya Mwananyamala.
Tathmin ya mwaka jana inaonyesha benki ya KCB ilitoa misaada yenye jumla ya thamani ya Tsh 362,545,000/= katika mchakato ufuatao:
• Tsh. 145,024,000- Sekta ya Afya
• Tsh. 130,000,000- Sekta ya Elimu
• Tsh.73,521,000- Mafunzo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati (SMEs)
• Tsh. 14,000,000 - Sekta isiyo rasmi (jamii yenye shida mbalimbali kama vyakula, maafa n.k)
Mwaka huu tumetenga kiasi kikubwa zaidi cha fedha kwaajili ya kusaidia jamii inayotuzunguka katika sekta zilizotajwa hapo juu na mazingira nchini. Mikoa itakayofaidika ni pamoja na Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Morogoro na Zanzibar.
Hii inaonyesha jinsi ambavyo sisi KCB Bank tunavyozingatia wajibu wetu wa kusaidia jamii inayotuzunguka kupitia sekta za elimu, afya, mazingira na maafa mbalimbali ili kupunguza umaskini nchini.
Pia katika kusaidia jamii tumeenda mbali zaidi badala ya kusaidia tu kwa kutoa misaada mbalimbali pia tunayo akaunti maalumu kwa ajili ya mashirika na taasisi za kijamii yaani "organizations and institutions with social impact" akaunti hii inaitwa "community account" faida zake ni kama:
• Hakuna malipo ya mwezi ya uendeshaji ( no ledger fee)
• Hakuna kiwango cha kufungulia akaunti
• Uthibitishaji na upitishaji wa hundi za ndani bure
• Kupeleka fedha kutoka akaunti moja hadi nyingine kutoka KCB kwenda benki nyingine bure
• Yaani kwa ujumla uendeshaji wa akaunti hii ni bure kabisa – KCB Bank inachofaidi hapa ni pesa ya mteja ilyowekwa na kwa muda itakayokaa na benki yetu.
Hii akaunti ni mahususi kwa taasisi kama vile:
Hospitali, shule, vyuo, NGO, serikali za mitaa, manispaa, mashirika ya kidini, saccos , club mbalimbali n.k
Hivyo KCB Bank itafurahi sana ikiwa hospitali ya Mwnanyamala itafungua akaunti hii ili mpunguze gharama za uendeshaji mnazokatwa kwa mwezi katika benki zingine. Hata mkiamua kuanza na akaunti za project mlizonazo pia itakua ni jambo zuri kwa kuanzia. Kwa maisha yetu ya Kitanzania lazima tuwe na moyo wa uchungu na tujitahidi kupunguza matumizi yasiyoyalazima.
Akaunti zetu ziko nyingi ila leo tumechangua zile ambazo zinawalenga nyinyi moja kwa moja. Hivyo mbali na kipeperushi cha akaunti ya community ambacho kiko mbele yako kuna kipeperushi kingine cha akaunti za akiba za watu wazima wanafunzi na watoto; naomba mvisome kwa wakati wenu na mfanye uamuzi wa busara wa kufungua akaunti na benki ya KCB maana kuna akaunti nyingi nzuri ambazo hazipatikani mahali pengine nchini.
Ukitaka kufungua akaunti wewe piga simu tu sisi tutakufuata hapo ulipo na pia watu wetu wa mauzo watawatembelea ofisini kwenu ili kuwaeleza kwa ufasaha kuhusiana na akaunti zetu mbalimbali.
Karibuni sana na asanteni sana kwa kunisikiliza .

No comments:

Post a Comment

Tuachie Ujumbe wako hapa .