Taasisi ya Mkapa Foundation, inatarajia kujenga nyumba 700 za watumishi wa afya wanaotoa huduma katika maeneo ya vijijini.
Hatua hiyo inalenga katika, kuwaboreshea mazingira mazuri watumishi hao ili waweze kutoa huduma kwa ufanisi.
Hayo yalibainishwa juzi na Ofisa Mipango wa
Kitengo cha Uwezeshaji katika taasisi hiyo, Pamela Maro, alipokuwa
akizungumzia shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo katika kuboresha
huduma za afya vijijini.
Alisema lengo la ujenzi wa nyumba hizo ni kuboresha huduma kwa wananchi wa vijijini wanaokabiliwa na changamoto nyingi.
Maro alisema taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana
na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha kuwa changamoto
zinazowakabili wananchi wao vijijini zinatatuliwa.
Alisema mbali na kujenga nyumba hizo taasisi
hiyo pia imekuwa ikiisaidia Serikali kwa kuipatia watumishi wa afya na
kuwapeleka katika maeneo ya vijijini.
Alisema tayari taasisi imeshaisaidia Serikali
watumishi 230 wa sekta hiyo ambao wamepelekwa katika vituo mbalimbali
vya afya na hospitali za wilaya.
Ofisa huyo alisema katika kuhakikisha kuwa huduma
zinaboreka zaidi, taasisi imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa timu za
wasimamizi wa afya walioko wilayani.
Maro alisema mafunzo hayo pia yametolewa kwa wasimamizi wa vituo vya afya katika mikoa mbalimbali.
Alisema pamoja na jitihada hizo, lakini tatizo la uhaba wa watumishi katika vituo na hospitali mbalimbali ni kubwa sana.


I’m a Freelance Web Designer & Developer. I’m an enthusiastic, creative designer and geek with 3 years of strong commercial experience and a passion for creating beautiful, accessible websites using Web Standards
Bravooooo
ReplyDeletethat is whats app :)) :d (o) :)
ReplyDeletethat is great in deed
ReplyDelete