Marekani yachelewesha kombora la masafa

Monday, April 8, 2013



Wizara ya Ulinzi ya Marekani imechelewesha jaribio la kombora la masafa marefu lililotarajiwa kufanywa wiki hii katika jimbo la California, wakati kukiwa na ongezeko la mvutano wa nyuklia na Korea Kaskazini.
Ofisa mmoja wa Wizara alisema Waziri wa Ulinzi Chuck Hagel alipanga upya siku ya kufanywa jaribio la kombora hilo kwa jina Minuteman 3 litakalofanywa katika kambi ya jeshi la angani ya Vandenberg mwezi ujao.

Picha: Kumbukumbu za Kifo cha Kanumba.

Kaburi la Kanumba