Pinda kufungua kikapu
Tuesday, January 22, 2013
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda atafungua pazia la michuano ya mpira wa kikapu ya Kanda ya Tano itakayoanza saa 3 asubuhi kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Mussa Mziya aliliambia gazeti hili jana kuwa Waziri Mkuu Pinda atashiriki katika zoezi la ufunguzi litakaloanza saa 10 jioni uwanjani hapo.
“Mashindano rasmi yataanza saa tatu asubuhi na ufunguzi utafanyika jioni saa kumi,” alisema Mziya na kuongeza kuwa maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika.
Katika michuano hiyo inayoshirikisha mataifa ya Ukanda wa tano, Tanzania itawakilishwa na timu ya wanaume na wanawake, ambapo kocha wa timu ya wanaume, Bahati Mgunda amesema wachezaji wake wapo tayari kwa michuano hiyo.
Mgunda alisema licha ya kutojua wanaanza na timu gani, vijana wake wamejiandaa kukabiliana na timu yoyote ile na kusisitiza kuwa karibu nchi zote zinazoshiriki mashindano hayo wanajua uwezo wao.
Katika mashindano hayo, pia wachezaji kutoka vyuo vya Marekani na klabu za Canada, Morocco, Angola na Mexico watachezea nchi zao.
Nchi zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo ni Burundi, Rwanda, Djibouti, Misri, Kenya, Uganda, Somalia na wenyeji Tanzania.
Katika hatua nyingine, wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya wanaume na wanawake wametishia kutokushiriki mashindano ya Kanda ya tano ya Afrika kama uongozi wa TBF hautawalipa posho zao.
Katika kikao cha pamoja kilichofanyika jana katika Hoteli ya Traventine Magomeni, wachezaji wote wa timu hiyo wametoa muda wa mwisho wa viongozi wao kulipa posho zao kabla ya kuanza mashindano hayo.
Wachezaji wa timu hiyo kabla ya kuingia kambini walikuwa wakilipwa posho ya Sh6,000 kwa siku wakiwa mazoezini, lakini baada ya kuingia kambini fedha hizo ziliondolewa kabisa.
Mmoja wa wachezaji hao (jina tunalo) alisema kikubwa wanachodai ni posho zao na mavazi ya michezo ya kuvaa wakati wa ufunguzi.
“Tumechoka, hatukupenda kuongea na mwandishi wa habari kuhusiana na matatizo ya timu ya taifa, lakini imebidi ieleweke hivyo na tunataka Watanzania waelewe hivyo,” alisema mchezaji huyo.
Alisema,”inaonekana mchezo huu wa kikapu umeingiliwa na wanasiasa, ukiangalia hata ahadi zao walizozitoa kwa wachezaji nyingi hazijatimia.”
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa matatizo yote yamejitokeza kutokana na baadhi ya viongozi kujiweka pembeni na kumwachia kiongozi mmoja afanye kazi peke yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

I’m a Freelance Web Designer & Developer. I’m an enthusiastic, creative designer and geek with 3 years of strong commercial experience and a passion for creating beautiful, accessible websites using Web Standards
No comments:
Post a Comment
Tuachie Ujumbe wako hapa .